![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiq7tcw8G6XLtUyylMBEcPI1t2DjqRMsrjezvQN76c46DJmB18AgYvbcuyz2tUIK-MEjBarzZJ1XUp6l7nCV_l_uCninVsICPHNt_xs96pcxtKEcpFXAqT0Qox8EITrqK2n_9bKeBvT8cMV/s640/1435677582330.jpeg)
Azam FC inashusha wachezaji sita mahiri kwa
majaribio ya kujiunga na kuimarisha kikosi cha
msimu ujao ambacho pia kitawakilisha nchi
kwenye mashindano ya CECAFA Kagame Cup
wiki tatu zijazo na Kombe la shirikisho hapo
mwakani.
Wachezaji wanaokuja kwa mazungumzo,
majaribio na kupima afya zao kabla ya kujiunga
na kikosi cha Stewart Hall ni pamoja na
mshambulizi anayeongoza kufumania nyavu
kwenye ligi ya Zambia toka klabu ya Nkana Red
Devils Jimmy Ndhlovu ambaye awali alikuwa
akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Power
Dynamos.
Jimmy tayari amekuwa kwenye rada za vilabu
vingi vya Afrika Kusini hasa Morroka Swallows
ambao wanamnyatia hivi sasa.
Katika orodha hiyo yumo mshambulizi toka
nchini Uingereza Joe Dickson ambaye kocha
Stewart Hall anamfahamu vema kama ilivyo kwa
kiungo mchezeshaji Ryan Burge kutoka nchini
Uingereza pia.
Jean Baptiste Mugiraneza (Migi) ni kiungo
mwenye uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi
ya ulinzi kama ilivyokuwa kwa Mutesa Patrick
Mafisango.
Kwa sasa Migi anakipiga kwenye klabu bingwa
nchini Rwanda ya APR na timu ya taifa ya
Rwanda Amavubi.
Habari za ujio wa Migi zilikwisha vuja kwenye
baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda,
Uganda na Tanzania na sasa klabu ya Azam FC
inathibitisha kuwa mchezaji huyu wa zamani wa
Kiyovu Sports FC mwenye uzoefu mnchini na
mikikimikiki ya soka la Afrika Mashariki atatua
nchini baada ya kumaliza majukumu yake na
timu ya Taifa ya Rwanda.
Kama hao hawatoshi Azam FC pia inawaleta
magolikipa wawili wenye uwezo mkubwa na
uzoefu wa kutosha na mikikimikiki ya soka la
Afrika ili kwenda sambamba na vilabu
vinavyotamba barani Afrika, wachezaji hao ni
Vincent Atchouailou De Paul Angban kutoka
klabu ya Juanesse ya kwao Ivory Coast na
mlinda lango Mcameroon Nelson Bongaman toka
DCMP ya Kishasa DRC
Endelea kututembelea Mtandaoni Kupitia MJUMBE BLOG ili uzidi kuji update zaidi kila mara.
Post a Comment