Vuguvugu la kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM limeziidi kushika kasi ambapo Mh.Deo Filikunjombe ameendelea kuwafunika wagombea wenzake vibaya pale anaponadi sera zake kwa wanaccm na kupata mapokezi makubwa yanayoambatana na kubebwa juu na wananchi pale wanapofunga mikutano ya kampeni hizo.
Hali hiyo ambayo imejitokeza katika kata zote lakini siku ya jana katika kata ya Ludewa mjini hali ya kumshangilia na kumbeba ilizidi kwani umati wa wananchi uliofulika katika viwanja vya soko kuu la Ludewa mjini ulionekana ukishangilia na kumbeba juu kwa juu huku wakiimba Deo jembe letu.
Kutokana na hali hiyo inayotokea kila kata imewafanya wagombea wengine kukata tamaa wagombea hao ambao ni Kapteni Jacob Mpangala na Mhandisi Zefania Chaula ambao wamekuwa wakishuhudia matendo hayo yakitokea pale ambapo mwenyekiti wa mkutano ameshafunga mkutano.
Licha ya kubebwa na wananchi lakini Filikunjombe amelazimika kuwa mgombea wa mwisho kujieleza katika mikutano kutokana na wananchi kumsikiliza yeye tu na kutawanyika akiwa amekwisha jieleza bila kujali kuwa kuna wagombea wengine ambao wanapaswa kusikilizwa hivyo uongozi wa ccm wilaya umekuwa ukilazimika kumpanga kuwa wa mwisho katika kujinadi.
Azinadi sera zake katika ukutano wa mwisho ambao ulifanyika kata ya Ludewa Mjini Filikunjombe alisema kuwa chama cha mapinduzi kina ilani zinazotekelezeka hivyo wananchi wa wilaya ya Ludewa wanatakiwa kuzingatia mafiga matatu kuanzia rais ambaye ni Dkt.John Pombe Magufuli wabunge na madiwani.
Filikunjombe alisema kuwa maendeleo yaliyopatikana kwa muda mfupi wilayani Ludewa ni kutokana na umakini wa mbunge waliomchagua kupitia chama cha mapinduzi hivyo wananchi hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua vyama vingine kwani Dkt.Magufuli ni kiongozi makini hakuna asiyejua utendaji wake.
“upendo huu mnaonionesha mimi kama mbunge wenu ndio mnaotakiwa kumuonesha Dkt.Magufuli kwani bila yeye hata hizi barabara za lami za mitaa tusingezipata hivyo nawaomba mnichague mimi pamoja na madiwani wa ccm katika jimbo hili la Ludewa lakini rais wetu ni Magufuli na nawaomba wananchi wote msipoteze kura hata moja kwa vyama vingine”,alisema Filikunjombe.
Aidha mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Herman Luoga alisema kuwa wananchi wa jimbo la Ludewa hawana haja ya kuwa na mgombea mwingine wa chama cha mapinduzi kwani utendaji wa mbunge wao umekuwa ukionekana kwa macho na hata mikoa mingine inaujua utendaji wa Filikunjombe.
Bw.Luoga aliwataka wananchi wengine kutohangaika na vyama vya upinzani wakati mbunge wao anafanya kazi waliyomtuma awapo bungeni kwani kwa kujiunga na upinzani ni sawa na kusaliti kazi za kimaendeleo ambazo Filikunjombe amekuwa mstari wa mbele kuzitetea.
Mwisho.
Credit:Nickson Felix
Post a Comment