Julius S. Mtatiro added 4 new photos .
SAFARI YA MIAKA MITATU IMEKAMILIKA JUZI
(2012 - 2015):
Ndugu zangu, mwaka 2012 mwezi Oktoba
nilianza masomo ya shahada ya sheria (FULL
TIME) katika Chuo Kikuu cha TUMAINI DAR ES
SALAAM.
Juzi Jumatatu ndipo tumekaa kwenye chumba
cha mtihani (siku ya mwisho) kumalizia mtihani
wa mwisho wa mwaka wa tatu.
Nimepata uzoefu mkubwa sana kukutana na
walimu magwiji wa sheria kama Dk. Lamwai, Dk.
Sisty, Dk. Natujwa n.k. Lakini pia nimejifunza
masuala mengi ya kitaaluma kutoka kwa walimu
vijana chipukizi ambao wananoa bongo zao kuwa
madaktari wa kesho na kesho kutwa.
Tangu nikiwa mdogo nilitamani siku moja
kukamilisha ndoto hii muhimu, nimeendelea
kuikamilisha na nitaendelea kuitumikia. Naamini
siku moja nitakuwa mwanasheria mahiri, lakini
kwa ajili ya kuwasaidia wanyonge.
Wazazi wangu # Baba_Jane na # Mama_Verlena
wamekuwa msaada mkubwa sana kwangu, Dada
zangu Jane, Verlena na Sarah kwa kunisaidia
kujenga msingi wa elimu yangu ya nyuma kwa
michango ya hali na mali.
Napenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na
marafiki walionisaidia katika kuifikia ndoto hii.
Kwa mke wangu Zakia Hassan kwa kuwa nami
bega kwa bega kwenye hatua zote. Kwa watoto
wangu ambao walinikosa mara nyingi sana, wao
wanasoma na baba anasoma (Mara nyingi
wanangu huniuliza, Baba utamaliza shule lini?
Nami huwajibu ipo siku ntamaliza).
Kwa chama changu CUF na viongozi wake wakuu,
nawashukuru sana kwa kunipunguzia majukumu
ya uongozi tangu mwaka 2013 mwishoni na kisha
kuniruhusu nipumzike kabisa majukumu ya
uongozi mwaka 2014 mwezi Juni ili kuweka muda
mwingi masomoni.
Kwa dada yangu Judy Charl na mume wake
Wakili Msomi John Seka ambao wamekuwa
wakinitia sana moyo.
Kwa shemeji yangu Dkt. Hadija Jilala (PhD) kwa
kuendelea kuwa ROLE MODEL wangu kwenye
taaluma.
Kwa watanzania wote ambao mmekuwa mkinipa
moyo na kuniunga mkono na kwa wakosoaji
wangu ambao mmekuwa mkinisaidia kubadili
mienendo mibaya. Nyote nawapenda sana na
Mungu awabariki!
J. Mtatiro,
Dsm.
Post a Comment