Unknown Unknown Author
Title: WAGOMBEA WENZA NA FILIKUNJOMBE WAKIMBIWA NA WANANCHI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WANANCHI wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameanza kuwaadhibu wagombea wanaowania nafasi ya Ubunge na wanaompinga Filikunjombe kw...



WANANCHI wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe wameanza kuwaadhibu wagombea
wanaowania nafasi ya Ubunge na wanaompinga
Filikunjombe kwa kuwaacha peke yao katika
viwanja vya mikutano pale anapomaliza kujieleza
Deo Filikunjombe na kujibu maswali ya wananchi
wanapohitaji ufafanuzi.

Hali hiyo imeanza kujitokeza juzi katika kata ya
Ludende,Milo na Lugarawa katika mikutano
inayoitishwa na chama cha mapinduzi ili
kuwanadi wagombea watatu wa chama hicho
kwa wanachama ili kuweza kupiga kura za maoni
ambazo zitampitisha mgombea mmoja wa ccm
ambaye atapambana na wagombea wa vyama
pinzani.
Katika jimbo la Ludewa ndani ya chama cha
mapinduzi wamejitokeza wagombea wawili
wakipambana na mgombea aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo wagombea hao ni Mhandisi Zefania
Chaula,Kapten Jacob Mpangala na Deo
Filikunjombe ambapo hali imekuwa mbaya zaidi
kwa wapinzani wa Filikunjombe kwani
anapopangwa kuanza kujieleza Filikunjombe
wagombea wengine hubaki bila watu na kujikuta
wakibaki wao na viongozi wa ccm wilaya.
Mmoja wa wananchi ambao walitoka katika
mkutano wa hadhara katika kata ya Lugarawa
baada ya Filikunjombe kumaliza kujinadi kwa
wananchi.

Bw.Yusto Mgimba alisema kuwa
wananchi wamekuwa na shauku ya kumsikiliza
Filikunjombe na wamekuwa na imani naye hivyo
hawana mpango wa kuwasikiliza wengine kwani
hawajulikani kwa wananchi.

Bw.Mgimba alisema kuwa Filikunjombe bado
anakubalika na wananchi wa wilaya ya Ludewa
kwani maendeleo na ahadi alizoziahidi mwaka
2010 amezitekeleza pia wanafuatilia kazi
anazozifanya awapo Bungeni za kuwatetea
wananchi wake hivyo hakuna sababu ya
kubadirisha mbunge kama miaka mingine.

“tunawashangaa wagombea hawa wengine
wanavyotueleza watafuatilia miradi ya chuma cha
Liganga na makaa ya mawe ya Nchuchuma na
ujenzi wa viwanda vyake wakati kwa macho yetu
tumemuona na tumemsikia akifunga Bunge rais
wetu Jakaya Mrisho Kikwete akisema kuwa
mwaka huu atakuja kuweka mawe ya msingi ya
ujenzi wa viwanda hivyo sasa wao watafuatilia
wapi wakati kazi hiyo sisi wananchi tulimtuma
Filikunjombe na majibu tumeyapata?”

alisema
Bw.Mgimba.

Bw.Mgimba alisema kuwa wananchi hawaoni
sababu ya kuendelea kuwasikiliza hao wengine
wasiowajua hivyo wakishamsikiliza mbunge wao
ambao wanamkubali jembe lao wanatawanyika
kwani wanajua watadanganywa tu na hawa
wengine kutokana na ukweli kwamba hawana
jipya la kuwafanyia wananchi.

Aidha msimamizi wa mchakato huo wa kumpata
mgombea mmoja wa chama cha mapinduzi
ambaye ni Mnec wa wialaya ya Ludewa mzee
Hilaly Nkwera alisema kuwa mchakato
unakwenda vizuri na hauna kasoro kwani
wagombea wote wametulia na itabidi wakubali
matokea hata kama baadhi hawakubaliki na
wananchi.

Kuhusu wananchi kuondoka katika mikutano
baada ya Filikunjombe kumaliza kijieleza Mzee
Nkwera alisema kuwa suala hilo lipo na
inashindikana kuwazuia richa ya kuwa
wasimamizi wamekuwa wakitoa angalizo kwa
wananchi kutoa ondoka lakini imekuwa shida
hivyo imebidi wagombea wote wakubadliane kila
mkutano Deo Filikunjombe awe wa mwisho
kujieleza ili kuepusha hali hiyo.
Mzee Nkwera alisema kuwa makubaliano hayo
yanaweza kusaidia kwa upande Fulani ili
wagombea wengine wapate kusikilizwa sera zao
kwa wananchi kwani bila kufanya hivyo hali
itakuwa ni ile ile ya awali ya wananchi
kutawanyika baada ya kumsikiliza Filikunjombe na
kuwaacha wagombea wengine bila wasikilizaji.
Mwisho.
Credit: Nickson Felix

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top