Unknown Unknown Author
Title: MJUE MTANZANIA ALIYE TWAA MEDALI MBILI:SWAZLAND....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Swaziland baada ya kumvalisha med...

Bingwa wa mita 1500, Basil John kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akipongezwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Swaziland baada ya kumvalisha medali ya dhahabu katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland)


Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland.
Mwanariadha wa Polisi Tanzania, Basil John amefanikiwa kupata medali mbili za dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 1500 na mita 800 katika Michezo ya tisa ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) inayoendelea katika mji wa Mbabane Swaziland.

Mwanariadha huyo aliweza kuwashinda wanariadha wenzake baada ya kutumia dakika 1:49:00 katika mbio za mita 800 na katika mbio za mita 1500 aliweza kutumia dakika 3:49:02 na kuwaacha kwa mbali wanariadha kutoka nchi ya Zimbabwe na Swaziland ambao walionyesha ushindani mkubwa.

Mwanariadha mwingine kutoka Tanzania aliyeweza kupata medali ya dhahabu ni Fabian Nelson katika mbio za mita 5000, ambapo aliweza kutumia dakika 14:27:33 na hivyo kuifanya bendera ya Tanzania kupepea vyema katika michezo hiyo.

Ushindani mkubwa katika riadha upo kati ya Zimbabwe, Tanzania, Namibia na Swaziland ambapo nchi ya Swaziland imekuwa ikifanya vizuri katika mbio fupi.

Katika Michezo ya Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na Wanariadha kumi na mbili ambapo mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kuchukua medali 4 za dhahabu, mbili za fedha na moja ya shaba.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top