SENTENSI 50:LOWASA ALIPO HAMIA CHADEMA NA KUTANGAZA KUUNGANA NA UKAWA KULETA MABADILIKO...!
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ametangaza rasmi kukihama chama cha mapinduzi, CCM mchana huu na kutangaza kuhamia CHADEMA.....
Lowassa ametoa kauli hii Bahari Beach , Dar akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa UKAWA ambao wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia hatima yake kuelekea ikulu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Lowassa amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha, ameamua kujiondoa CCM kwa kuwa siyo baba yake wala mama yake na kuitikia wito wa UKAWA kupitia CHADEMA.
Amesema safari yake haitafanikiwa iwapo hawatajitokeza watu wengi kupiga kura na anaiomba tume ya uchaguzi iongeze muda ili watu wote waweze kujiandikisha
Lowassa amesema alinyimwa haki yake na CCM kama mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakuwa mnafiki akisema anaimani na chama hicho.
Baada ya maelezo hayo; Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe alisimama na kumkabidhi rasmi Lowassa Kadi ya CHADEMA.
Sentesnsi 50 Alizosisema Edward Lowassa Leo Wakati Akikabidhiwa Rasmi Kadi ya CHADEAMA.......
Yapo pia maneno ya Mbowe,Lipumba, Makaidi na Mbatia;fuatana nasi zaidi:-
1 Nimetumia wiki mbili kutafakari hatma yangu ktk Siasa, najua wengi wamesubiri kwa hamu.
2 Watu wangu wamesema fanya maamuzi magumu...
Namshukuru Mke wangu na familia wamekuwa na mimi katika kipindi kigumu-
3 Nawashukuru watu wengi waliojitokeza kuniunga mkono wakati natafuta wadhamini-
4 Uchaguzi wa Mgombea CCM ulijaa chuki dhidi yangu, Kamati ya Maadili haikutakiwa kuchagua Mgombea-
5 Kilichotokea Dodoma kinaitwa 'kubaka Demokrasia'
6 CCM iliwatumia vijana wachache kunikashifu na baadae wakapewa Madaraka makubwa
7 Kibaya zaidi kilikuwa kuwanyima Wagombea 38 wa CCM haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu
8 Nilinyimwa haki ya Msingi ya kusikilizwa na kujieleza CCM, nitakuwa mnafki kusema nina imani na CCM
9 CCM niliyoiona Dodoma sio CCM iliyonilea Kisiasa, mimi kama Mtanzania mwenye Uhuru nasema sasa basi
10 Mwalimu NYERERE alisema CCM sio baba yangu wala mama yangu,nimeamua kuanzia leo naondoka CCM na kujiunga CHADEMA
11 Namshukuru sana James MBATIA na Viongozi wa UKAWA kwa kuniamini na kunipokea.
12 Naamini UKAWA tutaondoa mfumo wa Utawala wa Chama kimoja, naomba Watz wajiunge nasi ktk SAFARI YA MATUMAINI
13 Naomba Watanzania wajiandikishe katika Daftari la Kupiga Kura,watunze Shahada za kupigia Kura ili tuiondoe CCM Madarakani
14 Mimi nauchukia UMASKINI, Kiongozi kujionesha maskini ni upuuzi. Natamani Watz wawe Matajiri kama MENGI na AZAM
15 Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?
16 Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?
17 Msiwatishe, kama wamefanya madhambi yao waambieni nimewasamehe mimi sitalipa kisasi..
18 LIPUMBA- 'UKAWA tumekubaliana maliasili na Rasilimali zitumike kwa manufaa ya Watz wote'
19 MBOWE- 'CCM imekuwa na Wabunge wengi ndani ya Bunge, imefanya waangalie maslahi yao zaidi kuliko Taifa
20 MBOWE- 'Tumekubaliana Wabunge wa UKAWA wakiingia Bungeni November 2015 waangalie zaidi maslahi waWatanzania'
21 MBATIA- 'Tunawakikishia Watanzania kwamba nguvu kubwa ya Serikali ya UKAWA itaangalia maslahi ya Watz'
22 Nilisema mtu ambaye ana ushahidi wowote kuhusu mimi kuhusika na RICHMOND peleka Mahakamani, kama huna kaa kimya
23 Tulikuwa na tatizo la Umeme, tukahangaika kuleta Mitambo ya kuzalisha umeme.
24 Tulipata taarifa kuwa mtu ambaye tunampa kazi ya kuzalisha umeme hakuwa na uwezo...
"Niliita kikao cha makatibu wakuu wanaohusika na richmond nikaagiza tuvunje mkataba. Mgonja akaomba aongee na simu baada ya one hr akaja na jibu mamlaka za juu zimesema mkataba uendelee"
Edward Lowasa 28/07/2015
"Kuhusu swala la Richmond Mwenye ushahidi aende mahakamani kama huuna ushahidi plz shut up and keep quite.
#Edward Lowasa
#zuiaGoliLaMkono2015
25 Niliondoka Madarakani lakini tatizo limeongezeka, mikono yangu ni misafi mwenye Ushahidi peleka Mahakamani
26 MAKAIDI- 'Nashukuru mmetuletea kifaa LOWASSA, nilimfahamu LOWASSA kupitia mtoto wangu
27 MAKAIDI- 'LOWASSA amekuja UKAWA afuate na Sisi tunavyotaka asahau kidogo mambo ya CCM'
28 MAKAIDI- 'Watanzania wamekwama, najua LOWASSA amekuja UKAWA kutukwamua.. Karibu sana LOWASSA'
29 Salum MWALIMU- 'Kuna taarifa kuwa sehemu kubwa ya Mikoa ya Mbeya, Singida na Arusha umeme umekatwa'
30 MBATIA-'Siku ya leo nina amani kutoka sakafu ya moyo wangu, ninawahakikishia Watz kuwa TZ bila CCM inawezekana'
31 MBATIA- 'UKAWA hatutamwaga damu lakini walio Madarakani wasituchokoze, uwezo wa kupambana kwa hoja tunao'
32 MBOWE- 'Tunapenda kumkaribisha LOWASSA pamoja na familia, marafiki zako na kundi la Watanzania wapenda haki'
33 MBOWE- 'Ujio wako CHADEMA umezua hofu nyingi kwa sababu hii ni nchi ya hofu'
34 MBOWE- 'Watu wengi wa CCM wamenipigia simu wakasema kumkaribisha LOWASSA ni kuharibu Chama'
35 MBOWE- 'Niliwajibu ni kweli ataharibu Chama, lakini nikajiuliza lini CCM ikawatakia mema CHADEMA?'
36 MBOWE- 'Kumleta LOWASSA kwenye meza hii haikuwa kitu chepesi, tumekaa Vikao viingi usiku na mchana'
37 MBOWE- 'Naongea kwa ujasiri,hatuwezi kufikiri mambo mema mapya kama tutaendelea kufikiri mambo mabaya ya zamani'
38 MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'
39 MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'
40 MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'
41 MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'
42 MBOWE- 'Hatujamkaribisha LOWASSA pekeyake, tumemkaribisha na Mamilioni ya Watanzania
43 MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'
44 MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'
45 MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakaribisha'
46 MBOWE- 'CHADEMA haiongozwi kwa kauli za MBOWE, inaongozwa kwa Katiba na Kanuni za Chama
47 MBOWE- 'Namshukuru sana Rais Jakaya KiKikwete mesaidia kutujenga Upinzani kuelekea Uchaguzi wa mwaka huu'
48 MBOWE- 'LOWASSA ujitahidi sana Mazoezi kwa sababu huku kuna mabomu'
49 MBOWE- 'LOWASSA alipokuwa analalamika Dodoma sisi tulikuwa tunafurahi'
50 MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakariuwezo...
Post a Comment