Unknown Unknown Author
Title: UPDATE KURA ZA MAONI JIMBO LA MBOZI NA VWAWA CHADEMA;TUME KUWEKEA HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Taarifa zilizo tufikia katika meza yetu hivi punde uteuzi wa awali nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Mbozi kupitia CHADEMA Mwalimu PASCAL ...


Taarifa zilizo tufikia katika meza yetu hivi punde uteuzi wa awali nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Mbozi kupitia CHADEMA Mwalimu PASCAL HAONGA APENYEZA KILELENI:


Matokeo ya awali jimbo la mbozi;

1. Pascal Haonga 82

2. Fred Haonga 34

3. Abdul Nindi 21

4. Sofia Mwabenga 8

5. A. Kabenga 4

Wengine hawajapata kura hata moja.

Zoezi la uchaguzi limekuwa huru na haki. Chadema mbele...."


Uteuzi wa awali jimbo la vwawa;

1. Fanuel Mkisi kura 136

2. Steven Mwamengo kura 42

3. Solomoni Kibona kura 22

4. Endrew Bukuku kura 9

5. Fadhiri Shombe kura 8

6. Dickson Kibona kura 5

7. Jonathani Mwashilindi kura 5

8. Furaha Mwazembe kura 3

9. Gift Kalinga kura 1

10. Jerwa Silwimba kura 1


Alicho sema Fanuel Mkisi;


"...wanajukwaa kama nilivyo waahidi kuwa leo ilikua kura ya maoni jimbo la Vwawa. Matokeo tayari niliwaahidi nikishinda au kushindwa nitawabriefu. Kati ya wagombea 14 nimeibuka kidedea kwa kupata kura 136 kati ya kura 251. Nawashukuru marafiki kwa kunitia moyo na kunishauri nasubiri baraka za kamati kuu...."


MJUE PASCAL HAONGA KWA UFUPI BIOGRAPHY YAKE TUME KUWEKEA HAPA:


Pascal ni nani?

Mtia nia jimbo la Mbozi Pascal Haonga ana jinasibu na kujipambanua kama mwanaharakati na mpambanaji aliye kieneza CHADEMA kwa hali na mali katika kila kata na zaidi ya vijiji 120 vya Jimbo la Mbozi kati ya 125 amesha vifikia kujenga chama.

Ana ibukia katika chuo kikuu cha Dar es salaam, kama anaye pigania masrahi ya wanyonge na watoto wa Masikini walio kosa mkopo!

Ana simamishwa masomo na wenzake kadhaa akiwemo Ernest Silinde!

2010 ana ungana na Mhe. David Ernest Silinde,kwenda kuligombania jimbo la Mbozi Mgharibi kama mwana CHADEMA kupitia vyuo vikuu.

Wana pambana kufa na kupona na kuibuka washindi kwa kumtupa mbali aliye kuwa Naibu waziri Siyame!

Baada ya uchaguzi mkuu 2010 ana endelea kukitumikia chama kama kiongozi wa kanda na mjumbe pia.

Kitaaluma Pascal Haonga ni mwalimu,aliye pata misuko suko mingi mno kutokana na kuonesha wazi misimamo yake ya kupinga uonevu majukwaani na katika semina mbalimbali!

Ikumbukwe ni Pascal Haonga, aliye fukuzwa katika semina ya sensaZhao ambapo wakiwa wame chukuliwa kama mawakala kupewa semina mpaka siku ya tatu walikuwa hawaja pewa posho wala stahiki zao zaidi ya kupewa semina...

Alifukuzwa ukumbini na kufutiwa ushiriki wake moja kwa moja wa semina hiyo Lakini mara tu baada ya semina hiyo walimu walio baki walipewa kila mmoja stahiki zake!
"Mbegu ili kufa ili iote upya"

Katika uchaguzi wa serikari za mitaa ana shiriki moja kwa moja kama Kampeni meneja kuwa nadi wagombea na wajumbe wa serikari ya kijiji cha Mlowo,na kuibuka kidedea kwa ushindi mkubwa na ulio tikisha wilaya nzima ya Mbozi kwani hawakupoteza mgombea hata mmoja!

Yeye ana semaje?
Akiongea na wajumbe katika kata mbali mbali jimbo la mbozi ame kuwa akisisiza kuwa "...NIME JIPIMA NIKAONA NINA TOSHA KUWA WAKIRISHA WANA MBOZI KATIKA ngazi ya ubunge...."

Anazungumziaje mtanange ndani ya chama chake,jimbo la Mbozi?

Kwanza ana amini CHADEMA Mbozi ni chama chenye taswira nzuri mno. Kina uzika vema na ndio maana watia nia 27 wame jitokeza kuchukua fomu ni ishara ya kupanuka kwa Demokrsia na wananchi kuwa na imani kubwa na CHADEMA...

ANAJIPA NAFASI GANI KATIKA WATIA NIA WOTE?
Tutashinda kamanda... Alisema mtia nia huyo!

'...Naiona nafasi ya kuwa wakirisha wana Mbozi wenye dhamira ya kubadilisha mfumo ulio tudumaza.'

Pamoja na changamoto za hapa na pale zinazo jitokeza likiwemo hili la baadhi ya wagombea kutoa rushwa na kuwa nunua wajumbe faragha ili wapewe ridhaa ya kupeperusha bendera ya CHADEMA Mbozi sitishiki.
Alisema.

Ana amini CHADEMA kwa chimbuko na asili yake sio chama cha watoa rushwa wapate uongozi wala wanao nunua wapiga kura huo ni mfumo wa chama kingine kabisa ambacho yeye anakiona kime jivisha magwanda ya CHADEMA.

Haamini kama matatizo ya wana Mbozi ni kukosa mbunge tajiri...
Kwani hata mbunge aliyekuwepo ni tajiri kuliko hata watia nia wote wa CHADEMA! Lakini ali amua kumpinga na kusema hawafai wana Mbozi kwasababu hawakirishi masrahi mapana ya wana Mbozi bali masrahi ya watu wake was karibu na madalali wanao ichuuza Mbozi kiuchumi kila siku.


Nashindwa kuanza kusema nitaifanyia nini Mbozi saizi kwani bado sija teuliwa kuwakirisha jimbo hili rasmi Lakini Madini ya kamaa ya mawe na Zao la kahawa na Hata vivutio vya kitalii havina manufaa ya moja kwa moja kwa wana Mbozi...
Alisema.

Ukiachana na barabara mbovu;
Pia miundo mbinu ya kijamii kama shule(Elimu),Barabara na afya nita sema nini ntakifanya nikisha pewa baraka na kamati kuu kuanza kunadi sera zangu.


Vipi kama kura za kukupitisha hazita tosha?

...kama nita shindwa kiuhalali bila mizengwe na rushwa kwa wajumbe nikajirizisha nita kubali matokeo!

Maana hatima ya yote hatutafuti ushindi wa Pascal Haonga bali tuna tafuta ushindi wa wana Mbozi kwa ujumla wao na CHADEMA...!

Lakini kama kuna mgombea atashinda kwa njia ya hongo sita muunga mkono kamwe.alisema mtia nia huyo.

Katika suala la KUJIAMINI nime jipima nina tosha...
Kupitia misuko suko niliyo ipitia.

Suala la kashfa na taswira yangu ndani ya jamii nina imani nayo kwani wana Mbozi wananitambua kama mwana harakati mpambanaji nisiye na skendo wala sio ndumila kuwili(ndimi mbili).

Suala la kujenga chama ndani ya Mbozi sina shaka nalo ni wazi kuwa hakuna mjumbe ambaye kweli kwa dhati haujui mchango wangu nime shiriki katika harakati kwa hali na mali kila mara ndani na nje ya Mbozi pia kuki pigania CHADEMA.

Rai yangu kama Pascal Haonga;
Wajumbe tafadhari hakikisheni mna teua mtu ambaye ana taswira njema kwa wana Mbozi! Awe mwenye maisha yanayo fanana na wana Mbozi wengi na aliye ishi nao katika kipindi chote asije akawa ana kuja leo lakini hayaishi Matatizo ya wana Mbozi anayaona kwenye Luninga na kuya soma kwenye mitandao ya kijamii au mwenye kashifa ndani ya jamii! Hata uzika na mtakipa wakati mgumu chama kushinda...

Nivema muwajue watia nia historia zao tabia zao na hulka zao.
Makamanda tume ya taifa ya uchaguzi ikitangaza kuligawa jimbo la mbozi basi mimi nitakuwa katika jimbo hili la Mbozi.


Stori na picha zote mali ya ofisi.

Pongezi kwa washiriki wote katika kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera ya CHADEMA jimbo la Mbozi na Vwawa!!


Zaidi ya yote HONGERA SANA PASCAL HAONGA!
Kamanda mpambanaji.

HONGERA FANUEL MKISI!


HAKIKA WAJUMBE MME WATENDEA HAKI WANA MBOZI!!

Salaam hizi zimfikie Godfrey Zambi na mawakala wake wote.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top