WAJUE WATIA NIA ISANSA WALIO WASHA KURUNZI MCHANA KWEUPE!
Jasta Mwanji;
Mtia nia udiwani kata ya Isansa akiomba apewe ridhaa ya kupeperusha bendera ya ukawa kwa tiketi ya CHADEMA.
ISANSA;ni moja kati ya kata zinazo unda jimbo jipya la la Mbozi kama lilivyo tangazwa rasmi na tume ya taifa ya Uchaguzi siku chache zilizo pita.
Kata ambayo katika wilaya pamoja na kuwa na mseto wa wakazi wake.
Shughuli za kiuchumi katika kata ya Isansa ni Kilimo cha zao la kahawa pamoja na kuwepo kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi na maharagwe pia.
Kata ya Isansa,Mbozi inachipuka miaka ya tisini ambapo nyumba za wakazi wake zina jengwa kisasa na kuezekwa kwa bati.
Miundombinu kama barabara,zahanati na shule zina ongezeka kwa wingi.
Wakazi wake wengi katika kila baada ya kaya kadhaa wana miliki vyombo vya moto.
Uchumi imara na watu wana wekeza zaidi kwenye zao la kahawa ambalo katika zama zile lilofananishwa na dhahabu.
ISANSA ina pokea makampuni na mashirika mbalimbali kwa ajili ya ununuzi wa kahawa pia wageni kwa wingi wanatumia fursa hiyo kuhamia na kuomba ukazi wa kudumu katika vijiji mbalimbali ndani ya kata hiyo.
Wafanyakazi mbalimbali pia wana anza kuwekeza mitaji yao kwenye kilimo na ununuzi wa zao la kahawa.
Wenyeji wake wakarimu na wenye maisha yenye uasili na mfumo wa kichifu katika koo mbalimbali una nasibiwa kama njia ya uongozi.
Sherehe na ngoma za asili kama Lipango,Mbeni,Mang'oma,Mampenenga na mfumo wa dini za kigeni zina pokelewa na kuenezwa na wakazi wake.
Katikati ya jamii ya miaka ya themanini kina zaliwa kizazi kipya...
Katika uzao huo pia anazaliwa Jasta Mwanji;
Ana yaishi maisha ya wana Isansa maisha ya neema yale maisha ya Maziwa na Asali.
Maisha ambayo kama ukijitambulisha kuwa una tokea Isansa Mbozi basi una maanisha MAISHA BORA...
Kizazi hicho pia kinatoa wana wa nchi wengine kama JONA KYEJO;wana ionja Isansa yao wana ifaidi kama jamii.
Elasto Mbella Ngaya;ana yaonja pia matunda ya Isansa ya wote...
Aron Sinka;ni miongoni mwa walio yaishi maisha na kufaidi neema ya Isansa.
Wapambanaji na wana mabadiliko walio amua kjng'amua suluhisho pekee la kesho ya wana Isansa.
Wame jikuta njia pekee ni KUYA PIGANIA MABADILIKO ya dhati.
Hamadi miaka 2000 Hali ya maisha ya wana Isansa ina pokwa na Umaskini ulio topea! Isansa ina kabidhiwa kwa madalali.Wana ichuuza Isansa na kuwa geuza wale wana Isansa walio jinasibu kama wakulima kuwa manamba wa mfumo mpya.
Akili za wana Isansa zina anza kubadilika na kuhama kutoka WAKULIMA BORA na kuwa BORA WAKULIMA...
Vijana wenyeji wa Isansa wana kimbia vijijini mwao na kwenda kigeuzwa vibarua mijini! Isansa haikaliki tena.
Haivutii kuishi kama zamani!!
Barabara mbovu na hazipitiki kirahisi.
Wakazi wake wengi wanajikuta katika mtanziko wa Sinto fahamu.
Vijana wanao maliza vyuo wanaonekana hawana faida tena...
Wame telekezwa na mfumo ulio amua kutengeneza matabaka.
Mfumo una wadhatirisha kwa kuwa geuza watumwa na manamba wa mawakala wa wanyonyaji...
Watoto wa kike wanapoteza thamani wana nunuliwa na mawakala na hata kudharirishwa ili waendelee kuutumikia mfumo huo!
Ina zaliwa Isansa mpya yenye Magofu na ambayo watu wake wana pima mazao yao kwenye madebe na wengine kuuza Mazao yao huku yakiwa shambani kwa madalali hao.
Kilimo hakina tija tena kime geuka shubiri....!
Wanao tambua wana amua kususia kilimo na kuchagua njia mbadala zaidi....
Isansa ime geuzwa kaburi!!
Ina meza ndoto za vijana wengi na wenye uwezo wana ikimbia na kwenda kuishi mbali ili kuikwepa dhahama hiyo!
Kizazi kipya bado kina ikumbuka ile Isansa ya zamani,Isansa ambayo kilimo ni tija kwa mkulima na sio kwa mawakala.
Kwa kuumiza Fikra na kusugua akili kwa umoja wao vijana wana kuja na majibu yakinifu.
Wana gundua kuwa ulio tufikisha hapa ni mfumo...
Mfumo wa kinyonyaji!!
Wana fanyaje basi??
WAME AMUA KUPAMBANA NA MFUMO HUO KWA KUAMUA KUWEKEZA NGUVU ZAO KWENYE DIRA YA UONGOZI UTAKAO MJALI MWANA ISANSA...
Endelea kututembea MJUMBE BLOG ili upate mikakati na mipango waliyo jiwekea na wanacho kifanya ili kuikomboa Isansa iliyo polwa na mfumo wa kinyonyaji....!
Nani atatuunganisha wana Isansa??
Jona Kyejo;Mtia nia katika nafasi ya ufiwani Isansa Ana amini Isansa sio mali ya WALANGUZI wana washa kulunzi mchana kweupee!!
Post a Comment