Bei za mafuta ya Petrol imepanda kwa Tsh 92/lita sawa na ongezeko la 4.91% ukilinganisha na mwezi uliopita.Kwa mfano hapa Arusha mwezi uliopita mafuta ya petrol ilikua ni Tsh 2,282/lita kwa sasa bei Tsh 2,374/lita
Ni neema kwa watumiaji wa Diesel ambayo kwa mwezi huu imeshuka kwa Tsh 17.5/lita sawa na 0.9% pamoja na mafuta ya taa yalioshuka kwa Tsh 29.27/lita sawa na 1.55% ukilinganisha na mwezi uliopita.
Sababu kubwa ya upandaji wa gharama ya mafuta ni mrundikano wa bidhaa kutoka nje kwenye bandari ya Tanga pamoja na gharama za usafirishaji kutoka hapo Tanga kwenda sehemu mbalimbali za nchi.
Maelezo Zaidi:
BEI ya mafuta ya petroli na dizeli huenda ikapanda maradufu, baada ya kuwepo kwa mpango kuukwepa Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS) katika kipindi cha kuelekea uchaguziu mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Hali hiyo imebainika kutokana na kuwepo kwa barua kutoka kwa Meneja Mkuu wa Uratibu wa Uagizaji Mafuta ya Petroli (PIC) Michael Mjinja kwenda kwa kampuni za uagizaji mafuta nchini.
Katika barua yake kwenda kwa kampuni hizo, Mjinja anasema mpango huo utaingia kwenye kipindi cha mpito kwa muda wa kuanzia Agosti hadi Novemba, mwaka huu.
"Kutokana na hilo, nahitaji kupata mahitaji yenu ya shehena ya mzigo mnayohitaji kwa kipindi cha Oktoba na Novemba," Ilisema sehemu ya barua hiyo huku ikitaka mahitaji hayo kuwasilishwa ofisi kwake hadi kufikia leo.
Alisema katika kipindi hicho kunahitajika usalama wa kutosha wa mafuta kwa kuwa kitahusisha kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hata hivyo, habari kutoka kwa baadhi ya wadau wa uagizaji mafuta walieleza wasiwasi wao kuwa kuna mpango wa kuzipendelea kampuni mbili ili zipate fursa ya kuagiza mafuta hayo kwa wingi na hata bei kupanda.
"Hii hatuikubali kwa kuwa kampuni zimewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika ujenzi wa miundombinu ya uagizwaji wa mafuta kwa pamoja hasa ujengaji wa matenki ya mafuta... serikali inapaswa kuingilia sauala hili haraka,''alisema mmoja wa wamiliki wa kampuni za mafuta.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, uamuzi wa kuandikwa kwa barua hiyo na kubadilisha mfumo wa uagizaji mafuta unapingwa na wadau wengi wa mafuta nchini.
Akizungumzia suala hilo, Mjinja alijibu kifupi kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kuridhia sheria za mafuta na gesi.
Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja uliratibiwa na serikali ili kudhibiti upandaji holole wa bei ya mafuta nchini na ukwepajio wa kodi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanya biashara wasio waaminifu.
Mbali ya hilo, mfumo huo ulisaidia kupunguza gharama kwa kampuni za uagizaji mafuta hasa zile za upotevu wa nishati hiyo na zile walizokuwa wakitozwa kutokana na meli kuwa nyingi na kukaa muda mrefu bandarini.
Kutokana na kuanza kutekelezwa kwa mfumo huo wa uagizaji mafuta kwa pamoja, gharama zilipungua kwa takribani dola za Marekani 37.33 kutoka dola 71.46 kwa tani moja ya ujazo.
Post a Comment