HII HAPA AIBU ALIYO IVUNA MTELA MWAMPAMBA MBOZI KWENYE KURA ZA MAONI!
Mtela Mwampamba wa tatu kutoka kulia pichani.
Wadau;
Nimepata taarifa kutoka kwa rafiki yangu wa karibu aishiye wilayani mbozi kuwa Mtela mwampamba amepata aibu kubwa mbele ya wana CCM wenzake baada ya kuambulia kura 18 katika mchujo wa kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi katika jimbo la Mbozi,aliyeibuka kidedea katika mchujo huo ni Godfrey Zambi aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo la mbozi mashariki.
Mwaka 2010 Mtela Mwampamba aligombea ubunge wa jimbo la mbozi mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA kabla ya jimbo hilo kugawanywa na kuwa majimbo 2,jimbo la mbozi na jimbo la Vwawa.
Katika uchaguzi wa mwaka 2010 Mtela Mwampamba aliweza kufanya vizuri na kujipatia umaarufu mkubwa,umaarufu uliomfanya ajioni kuwa yeye ni bora kuliko CHADEMA kiasi ambacho alifikia hatua ya kujisifu kuwa hata asipo pata ubunge kupitia CHADEMA ataupata hata kwa kupitia kwenye kingine....
Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu wilaya ya Mbozi Doris Kimambo;
Katika mchakato huo wa uteuzi wa mwakirishi wa jimbo la mbozi kupitia CCM,Naibu waziri wa kilimo na chakula ame ibuka kidedea baada ya kuwa shinda makada wenzake saba kwa kura 11286 akifuatiwa na Godfrey Mwenisongole aliye pata kura 4558 pia kada mwingine Paza mwamlima;alipata kura 2956 na Charles Chenza 2599.Wagombea wengine kura hazikufika 1000.
Post a Comment