Wajumbe wa Kamati Kuu wameingia ukumbini kwa muda wa dakika kadhaa zilizopita.
Hivi sasa Edward Lowassa anaingia ukumbini akiwa akiambatana na John Mnyika, Freeman Mbowe, Salum Mwalimu.
Tayari wamekaa meza kuu na wanasubiri kupewa ratiba. Mshehereshaji anamsifia Lowassa na kuwaambia wajumbe kuwa mabadiliko ni sasa. Wajumbe wanashilia na kusema Rais ni Lowassa 2015 -2020.
Wajumbe wanasimama na kuimba wimbo wa Taifa na baada ya wimbo wa Taifa unaoimbwa na timu ya Movement for Change viongozi wa dini watasimama na kutoa salamu.
Viongozi wa dini wanaenda jukwaani kwa ajili ya kutoa dua kukabidhi tukio hilo mikononi mwa Mungu kwamaana UKAWA wanaongozwa na Mungu kwa kila jambo.
Salim Mwalimu, anamshukuru Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, kuwa amehakikisha Ofisi ya Katibu Mkuu haikwami kwa lolote katika kutoa mafunzo ya kuwaandaa viongozi kuchukua dola.
Anasema wameimarisha kanda 8 za Tanyanyika kifikra na mtazamo kwa ajili ya kuandaa uchaguzi Mkuu na sasa wanaweza kusimamaia chama katika kila Kata Tanzania na pia anamsifia Mbowe kuwa katika eneo la usajili wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwaingia wanachama wapya waliokuwa nje ya chadema ili chama kipate ushindi.
Salim, anasema usajili uliofanywa na Mbowe wakati wa dakika za mwisho unastahili pongezi kwani wanaenda kushinda kwa kishindo.
Anasema uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana Chadema walifanikiwa kwa kiwango kikubwa licha ya kuwekewa mapingamizi katika baadhi ya maeneo nchini.
Amewashukuru wale wote waliojitoa kwa ajili ya kukipigania chama ili kiweze kuvuka salama na kushinda katika uchaguzi ujao wa udiwani, Ubunge, nafasi ya Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na nafasi ya Urais.
Mwisho anawakaribisha wageni wote walioshiriki mkutano huo wakiwemo wawakilishi wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi, mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini akiwemo, Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi wa Uganda Tanzania, Balozi wa Afrika Kusini Tanzania, Ubalozi wa Marekani, Ubalozi Rwanda Tanzania na wengineo wengi....
Anawakaribisha sasa viongozi wa dini akiwemo Mchungaji Kakobe, Gwajima, na Sheikh Katimba kwa ujio wao. Aanasema anatambua kuwepo kwa watu mbalimbali na muda wao kwa ajili ya kushiriki tukio hilo lakini hawezi kuwataja kwa majina yao kulingana na muda kuwa mdogo hivyo anawakaribisha sana.
Wajumbe wote wamesimama na kushangilia wakati Mbowe anasimama kuhutubia wajumbe wa mkutano huo.
Mbowe, anawashukuru wote waliojitokeza kushiriki mkutano wa wao leo, viongozi wa dini, mabalozi na wanahabari.
Mbowe, anasema "Leo tumekutana hapa Dar es Salaam ni siku muhimu kwa ajili yetu na hii itakuwa historia kwa nchi yetu"
Anasema anataka abadilishe mtiririko wa ajenda ili siku hii iwe ya kihistoria, anasema Tanzania ina ndoto ya mabadiliko ambayo inachagizwa na kazi kubwa iliyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema wakiwemo CUF, NLD na NCCR Mageuzi.
"Tunapopigania ndoto ya Taifa lazima tukubali kuwa umoja wetu usiotenganishwa kwa misingi ya kikabila wala misingi ya udini, tunawahitaji watanzania wote ili kwa pamoja tutekeleze ndoto ya mabadiliko katika nchi yetu"
Mbowe, anasema anaimani wameanza na Mungu na watamaliza na Mungu na katika utendaji wa miujiza anatenda kwa ajili ya chma hicho kwa makusudi na sio kwa bahati mbaya ili kulijenga taifa.
Anasema ili Taifa lipate mabadiliko ya kweli, kila mmoja aungane na UKAWA ili kulijenga taifa.
Mbowe, Anasema ushirika wao unamaana kama walivyokubaliana kwenye UKAWA kwamba wawe na mgombea mmoja wa urais katika mchakato huo na kwenye udiwani ili kuwepo na usawa.
Mbowe: Mabadiliko yanaletwa kwa kila mmoja wetu kujitoa. Tumepigana kwa miaka 25, watu wamepoteza maisha, wengine ni vilema.
Vyama vyote vya UKAWA vimepitia milima na mabonde.
Watu wa safari ya matumaini wameamua kuitafuta haki yao nje ya Chama chao.
Hata sisi CHADEMA tuna mapungufu yetu.
Wanachama ndio wenye CHADEMA, sisi tunatekeleza majukumu yetu.
Katika CHADEMA hakuna mwenye nguvu zaidi ya Chama.
Tunaomba wageni mliokuja chamani mje na mazuri ya chama chenu, yale mabaya hatuyataki.
Duni Haji, amejiuzulu Uwaziri wa Zanzibar na Umakamu wa Wananchi CUF.
Mheshimiwa Duni anasifa nyingi, amewahi kukaa kizuizini na Maalim Seif.
Duni Haji amehamia Rasmi CHADEMA.
Halikuwa jambo jepesi kumpata mgombea mmoja kwa tiketi ya UKAWA.
Baraza kuu, limewapendekeza Edward Lowassa na Duni Haji kupeperusha bendera ya UKAWA.
Mkutano Mkuu wa CHADEMA umempitisha Edward Lowassa kuwa Mgombea Urais na mgombea mwenza Duni Haji, hatimaye kuwa wagombea wa UKAWA.
CHADEMA imewapokea rasmi na kuwakabidhi kadi viongozi kadhaa mashuhuri waliokuwa CCM na ambao wamejiunga na CHADEMA.Wamekabidhi kadi viongozi wanne wanaowakilisha makundi kadhaa yaliyojiorodhesha kujiunga CHADEMA.Kadi ya kwanza imetolewa kwa Mgana Msindai Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mikoa wa CCM akiwakilisha wenyeviti kadhaa walioomba kujiunga CHADEMA.Kadi ya pili amekabidhiwa Makongoro Mahanga Naibu Waziri wa Kazi na Ajira kwa niaba ya mawaziri na manaibu waziri kadhaa walioomba kujiunga na jeshi la ukombozi.Kadi ya tatu imetolewa kwa Mbunge wa Arumeru Magharibi Ole Madeye akiwakilisha wabunge wengi walioomba kujiunga CHADEMA.Kadi ya nne imetolewa kwa Katibu wa fedha na Uchumi CCM Isaya Simon Bukakiye,Kahama ambaye anawakilisha viongozi wa wilaya kwa mamia ambao mpaka sasa wameorodhesha majina yao ili wasimame wahesabiwe!
Zinafuatia salaam kutoka kwa wawakilishi mbalimbali,vyama rafiki na wageni wengine...
Credit:Jf
Post a Comment