Jimbo la Mbozi ambalo lime kuwa likiongozwa na Mhe.Godfrey Zambi kwa miaka kadhaa sasa mhula huu wa uchaguzi pia wajumbe wame mpa Zambi Nafasi nyingine ya kuperusha bendera ya CCM kwa ushindi wa kura 11286,akifuatiwa na Godfrey Mwenisongole(4556),Paza Mwamlima(2956),Charles Chenza(2599) wagombea wengine watatu walipata kura chini ya 1000!
Ushindi huu wa Godfrey Zambi;Unampa nafasi nyingine ya kulitetea jimbo lake Zidi ya Wapinzani wake CHADEMA;Ambao katika kura za maoni Jimbo la Mbozi aliyeshinda alikuwa Ndugu Pascal Haonga.
Wachambuzi wa masuala ya siasa jimbo la Mbozi wana mpa nafasi ya ushindi Mgombea huyu wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA kubadili historia ya jimbo la Mbozi na kulitwaa upande wa Upinzani.
Jimbo pacha la Vwawa pia aliye pewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM ni ndugu Japhet Hasunga aliye pata jumla ya kura 10902 za wajumbe na kuwa acha mbali watia nia wenzake.
Nafasi hiyo ina mkutanisha na kijana machachari FANUEL MKISI;Atakaye peperusha bendera ya UKAWA pia kupitia CHADEMA katika jimbo hilo jambo ambalo mpaka sasa lime waacha njia panda makada na wafuasi wa CCM kwani hamu ya wananchi katika jimbo pacha hilo na Mbozi ni kuhitaji mabadiliko ambayo makada na wafuasi wa UKAWA wana amini umoja wao ndio ndio suluhu na jibu.
Wago
Post a Comment