Mbowe-Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sis tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.
Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.
Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.
Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.
Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.
Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko
Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho
Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi
Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua
Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.
Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.
Post a Comment