Wafungwa 6,000 wameachiliwa huru nchini Marekani katika jitihada za kupunguza msongamano katika magereza.
Kwa mujibu wa idara ya haki ya Marekani mpango huu unawalenga wafungwa waliopatikana na makosa ya kumiliki, kuuza na ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Hii ndio mara ya kwanza kwa idadi kubwa kama hii ya wafungwa kuachiwa huru nchini humo.
Idara ya haki inawalenga wafungwa ambao hawana historia ya kutumia nguvu ambao idadi yao inakisiwa kuwa ni nusu ya wafungwa wote nchini Marekani.
Takriban thuluthi moja ya watu wanaotarajiwa kuachiwa huru ni wageni na hao inatarajiwa kuwa watarejeshwa makwao.
Asilimia kubwa ya wafungwa hao waliachiwa huru ijumaa.
Kundi la pili la wafungwa litaruhusiwa kuondoka jumanne ijayo.
Post a Comment