Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rished Bade aliyesimamishwa kazi na Rais John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Rished Bade kuanzia Ijumaa.
Kwa mijibu wa taarifa za tangazo ambalo limetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Rais Magufuli amemsimamisha kazi kiongozi huyo wa TRA baada ya kugundulika kupitishwa Makontena zaidi ya 300 kinyemela katika bandari ya Dar es salaam.
Sakata hilo lilibainika wakati wa ziara ya ghafla ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa katika bandari ya Dar es salaam, Ijumaa.
Kwa mujibu wa taarifa za kusimamishwa kazi Bwana Bade, imedaiwa makotena hayo yameikosesha serekali ya Tanzania zaidi ya shilingi bilioni 80 za kitanzania.
Ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi, Rais Magufuli, amemteua Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt Philip Mpango kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa TRA mpaka uchunguzi utakapo kamilika.
Kutokana na kashfa hiyo, serikali imewaamuru maafisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka watakapopewa ruksa baada ya uchunguzi kukamilika.
Chanzo:VOA swahili
Post a Comment