Unknown Unknown Author
Title: NEYMAR TENA KWENYE HEAELINES..AMZIDI CHRISTIANO RONALDO...
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kufanya mipango ...

Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania
Cristiano Ronaldo kufanya mipango yake mingi na kwa asilimia kubwa kufanikiwa, miongoni mwa ishu alizofanya Cristiano Ronaldo kwa mwaka 2015 ni kuzindua movie ya maisha yake halisi, perfume, viatu vyake lakini hii sio taarifa njema kwake.

November 27 kutoka El Economista wametangaza kuwa kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike
imetangaza kumtaja staa wa FC Barcelona Neymar kuwa ndio staa namba moja kwa sasa anayeuza brand ya bidhaa zao, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Ronaldo kwa miaka kadhaa ila November 27 Neymar ndio ameandikwa kumzidi Ronaldo .

Stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa Neymar kwa mwaka 2016 ndio anatazamiwa kuwa staa atakayefanya vizuri kwa mauzo ya Nike na ndio maana kwa sasa anatajwa kuwa namba moja na
Ronaldo kushuka, licha ya kuwa
Ronaldo amefanya vizuri kwa miaka kadhaa. Ronaldo na Neymar wote wanamkataba wa kutangaza bidhaa za Nike .
source:milardayo.com

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top