Unknown Unknown Author
Title: MAARIFA YA JAMII:AMOS ASAJILE NA DHANA YA MAFANIKIO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
PERSONAL ASSESSMENT TOWARD SUCCESS.   Je unaweza Kuishi Interest/ Dream zako? Watu mbali mbali waliofanikiwa si kwa uwezo wao mzu...

PERSONAL ASSESSMENT TOWARD SUCCESS.
 
Je unaweza Kuishi Interest/ Dream zako? Watu mbali mbali waliofanikiwa si kwa uwezo wao mzuri wa kifedha tu lakini pia ni pamoja na kuishi interest/ dreams zao, wapo watu wengi huishi katika ndoto za watu kwa sababu vitu wavifnyavyo walichaguliwa ama kushauriwa na watu yawezekana pasipo wao kupenda, kutokana na sababu mbalimbali zilizojuu ya uwezo wao inawabidi kukubali, ukifanya kile kitu kinatoka ndani ya moyo wako au unamapenzi nacho uwezo wa kufanikiwa huwa ni mkubwa sana kuliko kushindwa. Amancio Ortega Gaona Tajili wanne (4) duniani, baba yake alikuwa akifanya kazi katika shirika la reli (a railway worker), ni mtu ambae alianza kuvaa nguo ambazo amedesign yeye mwenyewe kupitia kiwanda chake kidogo kutokana na ujuzi aliokuwa ameupate katika moja ya sehemu alizokuwa ameajiliwa, ameiishi ndoto yake mpaka sasa ni Spanish fashion businessman na founding chairman wa THE INDITEX FASHION GROUP. Amini kwamba unaweza

Kiwango chako cha uvumilivu kikoje? Thomas Edison Mgunduzi wa taa (Light bulb) Mwalimu wake aliwahi kumwambia “ni mtu mjinga asiyeweza kujifunza kitu chochote”, amewahi kufutwa kazi mara mbili kutokana na kutokuwa na mchango wowote katika makampuni husika, katika ugunduzi wake wa taa alishindwa mara 1000 lakini mwandishi alipomuhoji umejisikiaje kushindwa mara 1000 alijibu sijashindwa mara 1000 bali nimetumia njia 1000 kutengeneza bulb. Katika utoaji huduma/biashara zutu yapo mambo mengi sana huweza kutukatisha tamaa/kuturudisha nyuma/kutuyumbisha na kutuvunja mioyo kabisa na hivyo kutamani ndoto zetu zife, yatupasa kuwa wavumilivu maana njia ya mafanikio si lele mama hata kidogo.

Yapo mambo matano ambayo nitapenda kushare nanyi kama vitu ambavyo unaweza kutumia kujiuliza au kujiimarisha katika njia ya mafanikio uiendeayo, keep on touch for other three things.

Amos Asajile,
3/12/2015.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top