Unknown Unknown Author
Title: MAGUFULI:HAKUNA MFANYA BIASHARA ALIYE NICHANGIA KUINGIA IKULU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Osca Mwapinga shared Times Fm TZ 's photo . 18 mins · Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyem...
Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, ili aweze kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi kwa faida ya wananchi.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta binafsi, katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa ( TNBC) kwa ajili ya kufahamiana.
Alisema wakati wa kampeni hadi kufikia siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu, hakupokea senti yoyote kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwa alijua akiingia madarakani anakwenda kufanya kazi tu.
“Nilijiepusha na fedha, mchango wowote kutoka kwa wafanyabiashara, kama yupo mfanyabiashara yeyote alinichangia hata shilingi mbili asimame hapa aseme, nilikwepa kwa sababu nilitaka iwe kazi tu,” alisema

 Credit:Times fm

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top