NEW YORK, MAREKANI
MKALI wa
muziki wa hip hop nchini Marekani kutoka kundi la Young Money Records,
Nick Minaj, amefanikiwa kumtoa kaka yake, Jelani Miraj, kifungoni baada
ya kulipa dola 100,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 200.
Jelani
alipelekwa jela kutokana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa
miaka 12, ambapo alianza kukitumikia kifungo tangu Aprili mwaka huu,
lakini msanii huyo alifanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya
kaka yake.
Nick
amekuwa akifanya makubwa kwa kaka yake ambapo kabla ya kwenda jela, Nick
alitoa mchango wa harusi ya kaka yake huyo wenye thamani ya dola 30,000
sawa na zaidi ya Sh milioni 60.
Hata
hivyo, msanii huyo alizidi kuonyesha upendo wa dhati kwa kaka yake
ambapo alimpa nyumba kwa ajili ya kuishi na mke wake mara baada ya
kufunga ndoa
Post a Comment