DAR ES SALAAM
Sekretarieti ya ajira kwa watumishi wa umma imefanikiwa kukamata vyeti 1,808 vya kugushi vilivyotumika kuombea kazi katika taasisi mbalimbali za umaa kati ya mwaka 2010 hadi 2015.
Sekretarieti hiyo imebaini kuwa vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vyuo vya ufundi stadi –VETA ndivyo vilivyoghushiwa zaidi na waombaji wa nafasi za udereva, hudumu na masjala katika taasisi mbalimbali za serikali.
Akizungumza jijini Dar es salaam, mkuu wa kitengo cha mawasiliano sekretarieti ya ajira kwa watumishi wa umma, Riziki Abraham amesema udanganyifu huo haujajitokeza sana kwa waombaji wa nafasi za uhandisi, madaktari na uhasibu.
Riziki amesema serikali imeanza operesheni maalum ya kukagua vyeti vyote vya watumishi wa umma na waombaji wapya watakaobainisha kufanya udanganyifu watafikishwa kwenye vyombo vya dola
Naibu katibu kitengo cha tehama sekretarieti ya ajira, Samweli Tunganye amesema kuwa matumizi mabaya ya madaraka, kukithiri vitendo vya rushwa, na uwajibikaji mbaya ni maeneo makuu ya kushughulikiwa na serikali ya awamu ya tano.
CREDIT:JOSEPHINE MWAISWAGA / ALEX
Post a Comment