
Na: Yericko Nyerere
Tanzania itapata dola 12 kwa ujazo wa pipa moja la mafuta kutoka serikali ya Uganda, itakapoanza kusafirisha mafuta hayo kwa bomba hadi Bandari ya Tanga. Dola 12 kwa ujazo wa pipa moja ni sawa na 2o% ya mauzo ya mafuta kwa pipa ktk soko la dunia.
Bomba hilo linatarajiwa kusafirisha ujazo wa mapipa 140,000 kwa siku. Hii inamaana kuwa kwa siku Tanzania itapata dola 1,680,000 kwa siku. Kwa mwezi chukua $ 1,680,000 x 30 = $ 50,400,000. Kwa mwaka $ 50,400,000 x 12 = $ 604,800,000.
Dola 604,800,000 ni sawa na Shilingi Trilioni 1.5 za kitanzania kwa mwaka. Kwahiyo Tanzania itaingiza Trilioni 1.5 kila mwaka kutokana na bomba la mafuta. Yani mapato yatokanayo na bomba la mafuta yatazidi mapato yatokanayo na sekta zote za uchumi nchini isipokuwa mapato ya sekta ya utalii. Trilioni 1.5 ni sawa na asilimia 5.1% ya budget yetu kwa mwaka.
Kazi nzuri ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ndio imezaa mradi huu na kuzuia usiende bandari ya Mombasa. Hongera sana TISS kwa kufanikisha mpango huu wenye faida kubwa kiuchumi. Kwenye kitabu cha "Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi" kilichoandikwa na Yericko Nyerere ameshauri namna Idara ya Usama wa Taifa (TISS) inavyoweza kutumika kwa maslahi ya kiuchumi kwa taifa badala ya kutumika kisiasa na kuwatumikia wanasiasa.
@Yericko Nyerere
Post a Comment