Unknown Unknown Author
Title: KUTO CHUKUA MSHAHARA KWAMPONZA BOSI WA TIC!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Bi. Juliet Kairuki ametumbuliwa kwa kosa la kutokuchukua mshahara. ALIYE TUMBULIWA...


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Bi. Juliet Kairuki ametumbuliwa kwa kosa la kutokuchukua mshahara.



ALIYE TUMBULIWA TIC NI NANI??
Julieth ni mke wa Dr. Kairuki ambaye ni Mkurugenzi wa Mikocheni Hospital. Kabla ya kuja Tanzania alikuwa akifanya kazi South Afrika akilipwa mshahara wa USD 15,000.

JK ndiye aliyemkuta South Africa akamuomba arudi nchini kuja kusaidia pale TIC baada ya Mkurugenzi wa kipindi hicho yaani Ole Naiko kustaafu.
Taarifa zinasema, Kabla Julieth hajaja Tanzania, alihitaji mshahara wake usiwe chini ya milioni 18. Ikumbukwe South Africa alikuwa akilipwa 15K USD sawa na shilingi milioni 35. Kwa hiyo kukubali kulipwa milioni 18 ni kukubali kupunguza milioni 17 kitu ambacho si rahisi kwa watu wengi.
Alipofika nchini TIC wakamwambia katika malipo ya mishahara, hawana scale ya milioni 18, wakataka kumlipa milioni 5. Julieth akakataa.
Yaani kutoka mshahara wa milioni 35 kule South Africa hadi milioni 5?? Akamwomba JK arudi South Africa kuendelea na kazi yake, lakini JK akaagiza TIC wafanye marejeo na maboresho katika mishahara yao ili kuweza kumlipa Julieth.
Kwa hiyo Kipindi chote hicho alikuwa hapokei mshahara kwa sababu alikuwa hajafikia MAAFIKIANO na serikali. Sasa kabla TIC hawajakamilisha marejeo na maboresho ya mishahara ndio JPM akawa Rais. Akawa na slogan yake ya kubana matumizi.
Kwa hiyo TIC wakaogopa kuendelea na marejeo na maboresho ya Julieth Kairuki. Katika ufuatiliaji JPM akaambiwa kuna Mkurugenzi hajapokea mshahara tangu 2013 hivyo akatengua uteuzi wake!
Hapa lazima tujiulize:
1. Aliitwa kuhojiwa??
2. Baada ya maamuzi haya, nani wa kulaumiwa??
3. Walio toa taarifa kwa Rais walimpa taarifa yote au nusu nusu??
MY TAKE: Kuna laana inaweza kulikumba taifa kama utumbuaji wa majipu hautakuwa na utaratibu maalum na umakini wa hali ya juu. Kuna watu wataonewa kwa sababu hawana mahali pa kujitetea wala kukata rufaa!
**naomba kukosolewa kama kuna mahali nimekosea**
Charles Francis M,
"Caytano Maytano" daima!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top