Unknown Unknown Author
Title: ASKARI WA FFU JELA MIAKA 30,VIBOKO 12 NA FAINI YA FEDHA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA SEKONDARI....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha ni kutoka kumbukumbu za Maktaba ya MJUMBE BLOG haihusiani na tukio. ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Raphael Mako...
Picha ni kutoka kumbukumbu za Maktaba ya MJUMBE BLOG haihusiani na tukio.

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Raphael Makongojo (25) aliyembaka aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Pia Makongojo amepewa adhabu kali, ikiwemo viboko 12 pamoja na kuamriwa kutoa faini ya Sh milioni 15 mara atakapomaliza kifungo chake.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Arusha ndani ya chumba cha faragha (chemba) ambako waandishi hawakuruhusiwa kusikiliza hukumu, lakini baadaye waliambiwa kwa sharti la hakimu wala waendesha mashtaka kutajwa majina yao kwa sababu kesi hiyo iliendeshwa faragha.
Awali kesi hiyo ilianza kwa mshitakiwa kusomewa maelezo yake ya awali akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe ambaye hivi sasa amemaliza masomo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top