Pichani kutoka kushoto ni Diwani wa Viti maalumu Bi Mbaya Isabela ambaye ni mwenyekiti wa wanawake wilaya,Anaye fuatia ni Ndugu Barton Sinyenga Diwani wa Ipunga,Mhe.Richard Mahaya(Katikati),Mwenyekiti wa kamati ya shule ndugu Godfrey Mwamlima mwishoni kulia ni Mhe.Emily Mzumbe
Pichani ni mwonekano wa Mbele darasa na ofisi zilizo ezuliwa kama zinavyo onekana picha katika shule ya Msingi Lungwa.
Pichani ni iliyo kuwa ofisi ya walimu shule ya msingi Lungwa,Mbozi
Pichani ni mwonekano wa lililo kuwa darasa la pili katika shule ya msingi Lungwa,Mbozi.
Jengo lililo ezuliwa na Mvua Mwonekano wa nyuma kutoka kushoto ni darasa la Pili na kulia ni iliyo kuwa ofisi ya walimu.
Pichani ni iliyo kuwa ofisi ya walimu shule ya msingi Lungwa,Mbozi
Pichani ni mwonekano wa lililo kuwa darasa la pili katika shule ya msingi Lungwa,Mbozi.
Pichani ni Mwonekano wa shule ya Msingi Lungwa,kama inavyo onekana upande wa pili ndani,
Mwonekano wa majengo ya shule ya msingi Lungwa kwa mbele
Neno la shukrani kwa walio jitolea kukamilisha ujenzi wa ofisi ya walimu Lungwa,Mbozi
WACHACHE LAKINI BORA::
#LUNGWA ma Home Ville::
Lungwa shall Never Die....
#Our_Home_land or #Die.
Swali Lungwa ni nini?
Jibu:Lungwa ni mimi,
Lungwa ni sisi,Lungwa ni damu za watu,
Lungwa ni kila uzao ulio hai una ishi na ulio matumboni au kwenye miili yetu au ulio kaburini chini ya aridhi.
Jana nilishiriki kwenye harambee ya ujenzi wa Ofisi ya walimu kijijini kwangu (ambako ndiko liliko chimbuko langu),Lungwa.
Nimezaliwa nikaikuta shule hii,
Nime ishi kwenye mazingira ya shule hii zaidi ya miaka kumi,
Nime anza darasa la kwanza 1995 mpaka la saba 2001.
Nlipewa taarifa za kuezuliwa kwa ofisi ya walimu na darasa moja,ambalo lilikua lina tumika kama darasa la pili(ambalo mimi nilitumia kama darasa la tatu,kabla sija jiuzulu kwa ridhaa yangu umonita wa darasa).
Nilipo wasiri eneo la tukio mida ya saa sita mchana,siku ona mtu na harambee ilitakiwa ifanyike saa saba mchana,nilikaribishwa na waaandaji ukumbi wawili na Mwenyekiti wa shule tu ndugu Godfrey Mwamlima.
Hata muda wa harambe ulipo wadia(yapata saa kumi na nusu),Vijana wa rika langu nilio waona walikua hawazidi watano,na wazee wa makamo yapata Ishirini meza kuu watano pia.
Ni jumla hiyo ya watu thelesini ukumbini iliyo anza kunitia hofu,
Nikajisemea Wanakijiji cha Lungwa,walitaka nani aje awajengee shule yao??
Lakini muda wa kuchangia ulipo wadia nilishangazwa na hamasa ya walio jitokeza kwenye harambee ile,
Hakika nilijisemea moyoni kua WACHACHE LAKINI BORA!!
Asikwambie mtu wanakijiji wale walifikia Malengo yao kwa zaidi ya asilimia tisini.
Kwenye jengo la ofisi ya walimu(Jengo lililo kua shabaha kuu) kwa harambee ya jana tu lilikua limesha kamilika,
Jengo lililo bakia ni darasa la pili lililo ezuliwa pi.
Hilo ni deni kwa wana Lungwa.
UKITOA MWANA LUNGWA HAKUNA MTU ATAKAYE WALETEA Majengo kwenye maboksi,
Lazima tujitoe wenyewe,kwa hali,mali na nguvu zetu.
Huu ni utamaduni mzuri,Utamaduni wa kuamini katika uwezo wetu kwanza.
MAJINA YA WALIO JITOLEA SEHEMU YA MUDA WAO,NGUVU ZAO,MALI NA HALI ZAO YATAKUMBUKWA DAIMA.
Majina haya yata ishi na ni nuru kwa wakaaji wa Lungwa,na majirani zake.
TUSITEGEMEE WATU WACHACHE wenye fedha wajitoe kujenga mahali ambapo watoto wetu hasa wa tabaka la MASIKINI watapatia ELIMU.
Na hata kama wakijitokeza,Tuwaombe watupe ridhaa tuchangie kwanza sisi(Sisemi tukatae michango yao,Tupokee lakini Kamwe TUSIJE TUKA JIWEKA PEMBENI sisi wenyewe.
Lungwa ni yetu,Lungwa sio mali ya mtu,
Kila mwana Lungwa ajitoe,
Kwa manufaa ya Lungwa,
Leo shule kesho inaweza kuwa Zahanati,
Daraja au Kivuko.
Asanteni.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU Kibariki kijiji cha Lungwa,
#MJUMBE_Sr
Picha zote za kumbukumbu mali ya Mpiga picha wetu
Post a Comment