Unknown Unknown Author
Title: MADUDU TASUBA YAMAFUMBUA KINYWA VITALI MAEMBE;AJIKUTA MIKONONI MWA POLISI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
1980s ; Baba mzazi (Mwl. Khalfani Matitu) akiwa na mwanafunzi wake kutoka nchini Uingereza (Andrews) katika viunga vya kilichokuwa Chuo C...


1980s ; Baba mzazi (Mwl. Khalfani Matitu) akiwa na mwanafunzi wake kutoka nchini Uingereza (Andrews) katika viunga vya kilichokuwa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TaSuBa). Nasikitika sana kusikia taarifa zinazokichafua chuo na kuiharibu heshima yake! Chuo kina idadi kubwa tu ya Walimu na Wanafunzi wasio na sifa! Sasa tutapata matunda gani? Tunaposema sifa, hatuzungumzii elimu tu kwani hapo zamani palikuwa na wakufunzi wenye elimu ya msingi tu lakini walifanya vema! Ifahamike kwamba hawa walikuwa walimu maalum na wenye kujua wajibu wao. Chuo kimekuwa kichaka cha wezi! Hii ni aibu na haikubaliki hata kidogo, Ikiwezekana ni lazima wahusika watumbuliwe hata kwa nguvu ya umma. Chuo hiki ni hifadhi ya wanaBagamoyo ambacho kwamiaka mingi kilituletea heshima kubwa sana, ilikuwa ni furaha kusema "Natokea Bagamoyo -Sanaa ilipo"
Viongozi wa sasa si tu wanakosa elimu, lakini pia hekma na busara za utendaji wa kazi, nadhani hawajui wajibu wao na pia hawajui misingi ya chuo cha sanaa. Mimi binafsi nimekuwa na kuziona nyakati pendwa za chuo, nimecheza ngoma na kuruka sarakasi! Hivyo hakuna mtu atakayenidanganya. Lazima vijana wenye elimu, uwezo na uzoefu wakiendeleze chuo, la sivyo itabaki kuwa historia yakwamba paliwai kuwa na chuo cha sanaa Bagamoyo kama ilivyo sasa.‪#‎ChuoChaSanaaKichakaChaWezi‬! Tag your friend and let them know that we are determined to fight for what is truthful ours! God bless you all



Haya ni maandishi yalio onekana kuumiza hisia za wahusika na ukamatwaji wa ndugu Vitali Maembe 
Tangu Chuo kianze haijawahi kufikia hatua hii mbaya kabisa kufanyiwa wasanii wanyonge!
Nyinyi wakina Nape Nnauye kwanini mnawafumbia macho wezi wa hawa?
Kadinde, Bwire na Kiiza vikao vyenu na Mkuu wa wilaya Bagamoyo kutafuta ufumbuzi wa Utapeli mlioufanya ndiyo mmeafikiana kuwaita Polisi waje wawapige Mabomu ya machozi Wanachuo TaSUBa mliowaibia?







Hiki ndicho alicho andika Julius S. Mtatiro
 Fikra za mtu hazifungwi kwa minyororo, fikra huishi milele hata mtu anapokufa! Na watu watakapozuiwa kuongea kabisa, hadi mtu wa mwisho, mawe yatasimama na kuongea, mawe! Mawe yatasema kwa niaba ya watu. Kwa hiyo, ni ujinga wa kiwango cha PhD kwa yeyote mwenye mamlaka hapa duniani, kudhani kuwa anaweza kuzibeba fikra za watu na kuzitia minyororoni, haiwezekani leo, haikuwezekana juzi na hatawezekana daima dumu.
Mtatiro J.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top