Unknown Unknown Author
Title: YERIKO NYERERE AZITAJA FAIDA NA HASARA ZA UJASUSI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kitaalamu kila binadamu anaweza kuwa ni jasusi! Kama utakuwa na utaalamu wa sayansi ya tabia za wanadamu, basi elimu au ujuzi wa...






Kitaalamu kila binadamu anaweza kuwa ni jasusi!

Kama utakuwa na utaalamu wa sayansi ya tabia za wanadamu, basi elimu au ujuzi wa ujasusi ni tabia ambayo ipo ndani ya nafsi ya kila mwanadamu, wanadamu wengi wana tabia za usiri na kujilinda kwa kila hali lakini pia ni wa dadisi. Sasa ukisha kuwa umefunzwa ujasusi rasmi unakuwa kama jasusi mkuu na inakuwa rahisi kujua hidden futures za huyo unaye mfuatilia au katika medani.
Ujasusi unakuja kuwa mchungu pale tu unapokuwa authozied kufanya hiyo kazi, kwani lolote linaweza kukutokea ikiwa ni pamoja na kudhuriwa na yule mhusika unayemfuatilia. Katika hali hii utachukuliwa kama msaliti na mnafiki hilo tu. Mara nyingi ukifanya ujasusi wa kiserikali na taifa lako likakutuma kwenda katika taifa lingine kufanya ujasusi, ikitokea ukakamatwa, taifa lako hukukataa katakata (in diplomatic) mpaka ujiokoe mwenyewe, lakini kukukana haina maana kuwa linakutelekeza kabisa, utaendelea kuwa under cover usije kuligeuka.... Hiyo ni kanuni ya high profile spy
Utamu wa ujasusi unapendeza na kuwa mtamu pale ambapo unaufanya kwa minajili ya mafanikio yako binafsi, kama biashara au kujilinda na maadui
Majasusi wengi huwa na akili za kufikiri na kutatua mambo kwa haraka mno, ni watu wenye maamuzi ya haraka, ni watu wenye weledi wa hali ya juu, huuliza maswali na kujenga hoja na ni wataalamu wa kusikiliza na kutambua lugha za picha au verbal communication, shafron, ni wazuri katika kutengeneza urafiki wa haraka au kuuvunja urafiki huo kwa haraka, sio waoga, wanauwezo wa kubadilika kulingana na hali yeyote ile, ni wajuzi wa kulinda hisia zao, wanapenda kujitenga au kukaa mbali na jamii, tabia nyingine ya hawa watu ni kwamba ni wasomi mno wengi wao wanauwezo wa kufanya kazi yoyote, yaani wana fani zote/ wanauwezo wakujifunza kitu kwa uharaka zaidi...
Hivyo basi binadamu akiwa na hizo tabia anauwezo wa kuwa jasusi ambapo akiutumia kwa manufaa yake anauwezo wa kufanikiwa kimaisha na kuwa na afya njema ama kusaidia taifa lake ikiwa litamtumia ipasavyo.

Na: Yericko Nyerere


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top