Katika nchi ya Kusadikika takwimu sahihi sio tatizo.
Wasadikika hua ni wajuzi wa kutengeneza UKWELI,La sio KUTAFUTA ukweli.
Maana wao wanaogopa gharama ya UKWELI.
Kuna wakati watu wa Magazeti tando "blogs" tunao tunza kumbu kumbu tumejikuta njia panda.Hata pale uunapo amua kutunza kumbu kumbu sahihi kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari unajikuta njia panda...
Hata unaye tunza hujui UKWELI ni upi???
Ukitunza Kumbu kumbu kama hizi,zenye mkanganyiko akaja akajitokeza Mzungu aka kwambia hakukua na Kumbukumbu sahihi za Historia yenu,ila Historia ya wazungu nchini kwenu mta pinga kwa hoja zipi?
Naaam,Yupi MKWELI? Hapo juu.
Hata mimi sijui,
Nilifundishwa KUUTAFUTA UKWELI!
Ifuatayo hapa chini ni Gharama ya UKWELI kama nilivyo ikuta kwenye menu::
UKWELI robo Utakufanya upoteze Cheo chako,
UKWELI nusu utapoteza ajira yako,
UKWELI kamili Gharama yake ni KIFO;Alisema Malcom X.
MJUMBE sr
Songwe,Mlowo
Kiwanda street
Post a Comment