Unknown Unknown Author
Title: SOKO MJINGA MLOWO SAFI TU:WATEJA SISI HATUNA TATIZO NA MTU NA WAFANYA BIASHARA NAO HAWANA MATATIZO KABISAA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
   Picha:Panaitwa Soko Mjinga,Mlowo Mwonekano wa Soko MmH! Mji mdogo Wa Mlowo Unakua kwa Kasi Kuliko Mikakati ya kiutekelezaji inayo fa...
   Picha:Panaitwa Soko Mjinga,Mlowo Mwonekano wa Soko

MmH!
Mji mdogo Wa Mlowo Unakua kwa Kasi Kuliko Mikakati ya kiutekelezaji inayo fanywa ili kupafanya wakazi wake wafanye Shughuli zao katika Mazingira Salama na Mazuri.
Unapo Ingia Sokoni Nikawaida kabisa ukikuta Wachuuzi wa Maparachichi,Nyanya,Vitunguu(viungo),mboga za Majani,Mazao ya Shambani(Mahindi,kabech,maharagwe),Samaki,Dagaa,Vitumbua,Maandazi Wauza Mitumba(Nguo na Viatu) Wakiwa wame mwaga Bidhaa Zao Chini na Mara nyingi Mvua ikinyesha Kuna kuwa na Topezito mno ambalo hutokana na Mazingira yalivyo,kwani hakuna Mikondo Rasimi inayo ruhusu Maji ya mvua kupita hivyo hutuama.
Unapo Tembelea Maeneo haya,kama ni mgeni unaweza uka dhani Hawa wachuuzi wana Fanya kazi kwa Mpito(Transt) kuna mahali baada ya siku chache wanatarajia kwenda kuanza Rasimi Kuweka Bidhaa zao;La hasha! Hawa Wapo hapa tangu zamani na hawana Mpango wa kuhamia kwingine.
Hawa ni miongoni mwa wafanyabiashara wengine wa Soko kuu la Mlowo ingawa wao wapo nje ya Soko kuu.Hufanya Shughuli zao Kila siku katika Madhingira haya Lakini hakuna Mikakati inayo fanywa kuhakikisha wanaboresha mazingira yao ya Kazi.
 Picha Ilipigwa kutokea Upande wa Pili,Mpiga picha amesimama Mpakani na Mabanda/Vilabu

Kinacho fanyika Hapa ni Kupunguza taka zilizo pembeni mwa bidhaa na kuzi hamishia kwenye dampo kuu ambalo nalo utokaji wake wa taka umekuwa Gumzo.Kamera yetu ime shuhudia mara kadhaa Dampo hilo likiwa limejaa kiasi cha kuzuia Mlango wa Soko kuu Kufunguka na kutiririsha Uchafu huku wahusika kila mmoja akimpigia dana dana mwenzake na kuchelea hali hiyo kwa miezi kadhaa na hata pale Siku walipo Zoa taka hizo Walizoa Nusu na nusu zika baki!


   Pichani ni Taswira Halisi ya Dampo la Soko(Mwekundu Kushoto) la Mlowo,Mlango wa Soko Umezuiwa na Taka Haufunguki!

Swali la Msingi;Wahusika wana mikakati gani ya kuhakikisha Madhingira ya kazi yao yana kuwa katika hali nzuri? Kwa kujenga Holi moja na kuwa kusanya wachuuzi wale Sehemu moja bora itakayo kuwa inatoa huduma ambazo sasa zina tolewa chini kwenye Tope/vumbi.Hilo ni wazo lakini lina weza kumbana na Kupuuzwa maana si kweli kwamba Wanao husika hawajui,Wanajua Lakini Wame puuza.Hawa nao ni miongoni mwa wateja au wauza bidhaa katika madhingira haya,kama sio wao basi ndugu na jamaa zao ndio tuna lipa gharama hizo.Gharama ya kufanya biashara katika mazingira ambayo kama ukipigwa picha unaogopa au una mchikia mpiga picha(Mweka Kumbukumbu).
Ashakumu si Matusi Ipo siku Watu wa Marekani watajitolea kuja kutengeneza madhingira ya Soko mjinga... Watatengeneza Soko ili wauza Maembe na Maparachichi nao wasiweke chini Maembe yao.
Nahitimisha kwa Kusema IPO SIKU.

MJUMBE Sr
MLOWO/MBEYA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top