Unknown Unknown Author
Title: MATUKIO KATIKA PICHA;WAANDISHI WA BLOG YA MBEYA YETU NA BOMBA FM RADIO WALIVYO JITOLEA KUKARABATI BARABARA YA BLOCK T,HUKU WAANDISHI WA JIJI WAKISHUHUDIA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hivi ndivyo Barabara ilivyokuwa kabla Waandishi wa Jiji wakiwa wamefika kuwashangaa wenzao wakiwa wanafanya kazi ya kutejenga ...
Hivi ndivyo Barabara ilivyokuwa kabla
Waandishi wa Jiji wakiwa wamefika kuwashangaa wenzao wakiwa wanafanya kazi ya kutejenga Taifa , wa pili kutoka kushoto ni Mwandishi wa Habari wa Bomba Fm Radio Richard Kamanga aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza Barabara hiyo akiongea nao.
Baadhi ya wamachinga na wananchi wa eneo hilo aibu zikiwa zimewashuka na kuamua kushirikiana na Waandishi wa Habari kutoka Bomba Fm  Radio na Mbeya yetu Blog kuendelea kutengeneza njia hiyo
Waandishi wa Jiji wakiahidi kuleta kifusi kwa ajili ya kurekebisha Barabara hiyo
 Wachina wakiwa wamefika eneo la tukio na kuahidi kuwa nao wataongeza nguvu katika ujenzi wa Barabara hiyo
Mchina akipata maelekezo juu ya Barabara hiyo
Hii ndio kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Mbeya yetu Blog sambamba na Bomba Fm Radio .

Picha na Mbeya yetu

********************
Wakati kazi ikiendelea baada ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuingia Mitini, na tukio hili kuripotiwa muda mchache uliopita kupitia Mtandao huu na Bomba Fm Radio huku waandishi hao wakiendelea ya kujenga Taifa ndipo Ghafla waandishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walipoweza kufika na kuwashangaa wenzao wakiendelea kupiga kazi na baada ya kuona aibu waliamua kuahidi kuleta kifusi kwa ajili ya matengenezo ya Barabara hiyo.

Nao Baadhi ya wamachinga wapenda maendeleo waliweza kujitokeza kwa ajili ya kuwaunga mkono waandishi wa habari walioanzisha kazi hiyo na kuwasaidia kazi inayo endelea ya ukarabati wa kipande hicho cha barabara.

Wachina nao hawakuwa mbali baada ya kusikia ripoti ya tukio hili wakaamua kufika kujionea wenyewe, na wao kuahidi kutoa mchango wao wa kuweza kutengeneza barabara hiyo.
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top