Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA JESHIAPONEA KIFO SOMALIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuch...


Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi
Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.
Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.

Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.
Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.
Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.
Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.
Chanzo:BBC

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top