FAHAMU:KUHUSU "CHE" GUEVARA!
Mara Kadhaa unaweza ukatembea mtaani ukakutana na Maandishi ya somekayo CHE!
Vijana wengi Hupendelea Kuvaa au hata kujisifu kuwa wao ni Wanaharakati kama CHE GUEVARA!
Je Unamjua?
Endelea Kusoma Zaidi.....
Ernesto Rafael Guevara de la Serna au Che
Guevara (* 14. Mei 1928 Rosario , Argentina; †
9. Oktoba 1967 La Higuera , Bolivia ) alikuwa
mtabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi
wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara
anajulikana zaidi kwa harakati zake za
kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko
Amerika ya Kusini na Afrika .
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara
alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani
ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe
umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na
maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi
wengi huku wachache wakiwa wanamiliki mali
za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili
hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa
umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi.
Aliamua kusoma kwa undani falsafa za Karl
Marx na baada ya hapo alijihusisha na harakati
za kisoshalisti nchini Guatemala chini ya rais
Jacobo Arbenzi Guzmán.
Mwisho mwa miaka ya 1950, Guevara aliungana
na Fidel Castro aliyekuwa akiongoza kundi la
kijeshi lililotwaa madaraka kwa nguvu nchini
Kuba mwaka 1959. Guevara alikuwa mmoja wa
viongozi wa serikali mpya ya Kuba. Katika
kipindi hiki, Guevara aliandika vitabu na makala
mbalimbali kuhusu nadharia na vitendo vya vita
vya msituni kwa nia ya kuondoa madarakani
tawala za kibepari na kibeberu.
Mwaka 1965 Guevara aliondoka nchini Cuba
akielekea Kongo-Kinshasa (hivi sasa inaitwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kwa siri
kusaidia harakati za kuondoa utawala uliokuwa
ukiongozwa na vibaraka wa mataifa ya
Magharibi chini ya Mobutu Sese Seko baada ya
kuuawa kwa Patrice Lumumba . Moja ya watu
ambao walifanya kazi na Guevara alipokuwa
nchini Kongo ni aliyekuwa baadaya rais wa nchi
hiyo, Laurent Kabila .
Guevara aliondoka nchini Congo na kuelekea
Bolivia ambapo alikamatwa mwaka 1967 na
jeshi la Bolivia likishirikiana na majasusi wa
Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA). Baada ya
kukamatwa kwake aliuawa kinyama.
Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama
nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya
kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina
ya Beret aliyopenda kuivaa vimekuwa kama
alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto
duniani.
Credit:Guda Guda
Post a Comment