Unknown Unknown Author
Title: ASILIMIA 80 YA MADINI YA TANZANITE YANA TOROSHWA N
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Asilimia 80 ya madini aina ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania, yanatoroshwa nje ya nchi na wafanyabiashara wasio waaminifu, huku...
Asilimia 80 ya madini aina ya Tanzanite
yanayozalishwa nchini Tanzania,
yanatoroshwa nje ya nchi na wafanyabiashara
wasio waaminifu, huku nchi ikiambulia
asilimia 20 tu ya madini hayo yanayozalishwa
eneo la Mererani mkoani Manyara.

Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Paul Masanja.
Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Paul Masanja, amesema
hayo wakati wa maonyesho ya kimataifa ya
Vito, yanayofanyika jijini Arusha na
kukutanisha washiriki zaidi ya 500, huku
kampuni 69 zikishiriki maonyesho hayo.
Masanja ametoa mfano wa mwaka 2013
ambapo Tanzania ilipata mapato yanayofikia
dola za Marekani milioni 38 kutokana na
Tanzanite, wakati Kenya walipokea Tanzanite
yenye thamani ya dola milioni 100, huku
India ikipata dola milioni 300 za madini hayo.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo,
serikali imeamua kujenga jengo la kuuzia
madini hayo na litakapokamilika hakuna
mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza
madini hayo nje ya jengo hilo kama ilivyo.
Credit:Eat5




LIKE page yetu MJUMBE BLOG Facebook au Tutembelee Mtandaoni kwa kuandika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo ili upate picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa Muhimu kila mara.


©Mjumbe Blog Volunteers

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top