Unknown Unknown Author
Title: HII HAPA NDIYO KASHFA MPYA INAYO IANDAMA SERIKARI YA TZ,HUKO ULIMWENGUNI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ikiwa bado Tanzania inakabiliwa na skendo ya pembe za ndovu zinazodaiwa kuondoka na ndege ya rais wa China alizuru nchini, kashfa nying...

Ikiwa bado
Tanzania inakabiliwa na skendo ya
pembe za ndovu zinazodaiwa kuondoka
na ndege ya rais wa China alizuru
nchini, kashfa nyingine kubwa
imezuka!
Tanzania inashutumiwa kurejesha
mpango wa kuwahamisha wamasai 40,000
katika eneo waliloishi kwa miaka na
miaka, ili kuipa eneo hilo familia
ya kifalme ya Dubai kwaajili ya
kuwinda wanyama.
Mwaka jana serikali ilidai kuahirisha
mpango wa kutenga eneo la kilomita
ya mraba 1,500 zinazotengenisha
mbuga ya wanyama ya Serengeti kwa
matumizi uwindaji wa biashara
utakaofanywa na kampuni yenye makazi
yake kwenye falme za kiarabu, Ortelo
Business Corporation (OBC).
Na sasa gazeti la The Guardian na
Uingereza na mengine, yameandika
kuwa mpango huo umerejea na wamasai
hao wameamrishwa kulihama eneo hilo
kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Wawakilishi wa wananchi hao
wanakutana na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, bungeni Dodoma kuelezea
hasira yao. Wanadai kuwa kuondolewa
kwenye ardhi hiyo ni kunyang’anywa
kwa urithi wao na maisha ya watu
80,000 yataathirika. Eneo hilo ni
muhimu kwa malisho ya mifugo ya
wananchi hao wanaoishi kwa kutegemea
ufugaji.
Serikali itawalipa shilingi bilioni
moja kama fidia ambazo wamasai
wamezikataa.
“Nahisi kusalitiwa,” mratibu wa
kikundi cha Ngonett Samwel Nangiria
ameliambia The Guardian.
“Bilioni moja ni ndogo saba huwezi
kulinganisha na ardhi. Imerithiwa.
Mama na bibi zao wamezikwa kwenye
ardhi ile. Hakuna cha kulinganisha
nayo.”
Msemaji wa wizara ya Maliasili na
Utalii, ameliambia gazeti hilo kuwa
hana taarifa kuhusiana na mpango
huo. Habari hiyo imeandikwa Jumatatu
kwenye magazeti na vyombo vingi
vikubwa vya habari duniani
likiwemo Daily Mail, rt.com ya
Urusi, eTurboNews, The Week Uk,
Europa Press, Ecoblog.it na vingine.





Tuna shukuru kwa kututembelea!



LIKE page yetu MJUMBE BLOG facebook au tutembelee Mtandaoni mara kwa mara Upate Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila Mara.

©Mjumbe Blog Volunteers

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top