
UZINDUZI WA KIVUKO DAR: Waziri wa Ujenzi,
Dk. John Magufuli leo amezindua kivuko kipya
cha MV Dar es Salaam chenye uwezo wa
kubeba abiria 300!.
Kivuko hiki kipya kitatoa huduma ya usafiri kati
ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa
Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo. Kivuko cha MV
Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko
chochote Afrika ya Mashariki na hasa
mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya
Kusini. Mia
By Qualcomm :
HAYAWI...HAYAWI...SASA IMEKUWA!
Leo Waziri wa Ujenzi Dk.Magufuli amekipokea
rasmi kivuko cha MV DAR ES SALAAM kama
utakvyokiona katika picha mbalimbali. Mbali na
Dk.Magufuli wengine waliohudhuria mapokezi
hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Saidi Meck Sadiki Saidi, RAS wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Balozi
Has.Mlango (Katibu Mkuu Mstaafu - Ujenzi)
ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA,
Mkurugenzi Mtendaji wa TEMESA, Kaimu
Mkurugenzi wa Bandari Mhandisi Matei,
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam
Itakumbukwa waziri Magufuli amekuwa
akiahidi kufanya jitihada za kupunguza
msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa
ni pamoja na kununua kivuko kitakachofanya
safari zake katika mwambao wa bahari ya
Hindi mpaka Bagamoyo.
Kivuko hiki mkombozi wa wakazi wa Jiji la Dar
es Salaam kimejengwa na kampuni kutoka
Denmark kwa gharama ya shilingi (Tanzania)
bilioni 7.9.
Sifa kubwa ya kivuko cha MV DAR ES
SALAAM:
1. Kina uwezo wa kubeba abiria kati ya 306
waliokaa hadi 400,
2. Kina spidi (speed) kubwa kuliko vivuko
vyote Tanzania na hata Afrika ya Mashariki
3. Kina ghorofa mbili (Two Floors)
4. Kwa ndani kina makochi mazuri kabisa ya
kisasa ikiwa pmoja na life jacket
5.Kina tekinorojia ya kisasa kabisa ya
Nivigation.
Picha za matukio mbalimbali pindi Dk.Magufuli
akikipokea kivuko:
credit:Jf
LIKE page yetu MJUMBE BLOG au Tutembelee Mtandaoni Upate picha,Matqngazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila mara.
©Mjumbe blog Volunteers
Post a Comment