
YA MAVAZI NA MITINDO MITINDO YA NGUO FUPI KWA DADA ZETU ninani aliye wabunia Ajira hii ya Vijana wetu wa Mtaani??
au Nayo ni shughuli??
"...makatazo kuhusu nguo fupi na marufuku ya kuonyesha maziwa hadharani ni mafundisho tuliyo letewa na Wageni,ambao walipo kuwa wakija kwetu utamadini wa kwao ulikuwa unakataza mwanamke kuoneaha hata kisigino na maziwa...
Huo ulikuwa ni Utamaduni uli itwa " VICTORIAN" kwasababu ulishamiri chini ya Malkia Victoria wa Uingereza...
Kwamba utamaduni wa Malkia wa Uingereza ndio ume fanywa kuwa Utamaduni wa Mwafrika ni kichekesho kichungu na ishara nyingine kwamba tume tekwa Akili na kisaikolojia.
...si nguo fupi pekee bali pia suruari zenye midomo mipana zilipigwa marufuku 'PECOS'..
Lakini kabla ya PECOS kujitokeza mjini,vijana wali anza kuvaa suruali "mchinjo" zilizo bana toka kiunoni hadi chini kiasi kwamba ulikuwa unajiuliza ni vipi suruari ina vuliwa na kuvaliwa.Ni kama vile mtu kashonewa suruari na siku ya kuivua itabidi ikatwa kwa mkasi.
Vijana wa chama waka ingia kazini kuwa saka vijana walio vaa "mchinjo" na ili kuwa shughurj nzito.Vijana walio vaa kinyume cha 'Utamaduni wetu' wali lazimishwa kusimama njiani na waka lazimika kuonesha kama chupa ya bia ina weza kupita katika mdomo wa suruali,la sivyo wana rushwa kichura.
Shughuli hii ili stishwa tu pale Mwalimu Nyerere alipo ikemea kwa kuita ya upuuzi.Katika mazungumzo ya faragha alisema:"Ninge kuwa kijana munge nikoma.Nyie si munataka kupitisha chupa moja.Mimi ninge shona suruali yenye kupitisha chupa tano,kisha nione mtafanya nini"
Baasa ya miaka mitano ndo ikaja pecos kama mwalimu alitabiri .
Kama ni kweli nguo fupi zina katazwa kwa mafundisho ya mawakala wa 'victoria',pecos zili katazwa kwa mafunzo ya nani??
Na:Jenerali Ulimwengu;
UTAMADUNI,DESTURI, MAPOKEO NA MABADILIKO;Raia mwema,Juni 27 2012!
UKWELI
Nitakua mtu wa mwisho kuwa Unga mkono wanao Wavua dada zetu wanapo vaa nguo fupi...
La sivyo waje hapa na Hoja za Msingi zitakazo nishawishi niamini nguo nyingi na defu au kubwa ndiyo Utamaduni wetu au Chimbuko letu!
Vinginevyo mimi nita Amini kuwa ni yale yale ya 'Shughuli' aliyo yaongelea Nyerere na Jenerali kwenye Rai yake Mwaka juzi.
Wana harakati hawa Tuwa katie viza ili waka Wavue nguo hata wale vigori wa Kwa Mfalme Mswati,ili Tukomeshe Utamaduni huu.
Picha hizo hapo ni Mavazi ya Mabinti wa Swazland kama Utamaduni wa Ki Afrika.
Tuna shukuru kwa kututembelea!!
Tutembelee mtandaoni andika MJUMBE BLOG ingia hapo au LIKE page yetu MJUMBE BLOG ili uji Update kila mara.
©Mjumbe Blog Volunteers
Post a Comment