Innocent Munyuku enzi za uhai wake.
MHARIRI Mwandamizi wa New Habari
Corporation, Innocent Munyuku amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini nyumbani
kwake Kimara jijini Dar es Salaam.
Ujumbe wa mwisho wa marehemu
Innocent jana usiku.
Baadhi ya marafiki wa marehemu wamethibitisha
kupitia mtandao wa Kijamii wa Facebook kuwa
wamewasiliana na marehemu usiku kupitia
mtandao huo ambapo meseji yake ya mwisho
akiwatakia usiku mwema ilikuwa saa 4: 23 jana
usiku.
Marehemu Innocent ni mmoja wa wahariri
wakongwe nchini na atakumbukwa sana kwa
ucheshi na utani wake.
Huu hapa ndio ujumbe wake wa Mwisho....
LIKE page yetu MJUMBE BLOG facebook au Tutembelee Mtandaoni kwa kuandika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo upate picha,matangazo,habari mpya,Taarifa mpya kila mara.
©Mjumbe Blog Volunteers
Post a Comment