
Wanawake wanasema na wanaume wanaovaa
long'i zao wakiwa wamezilegeza nao pia
wavuliwe
Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo
wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke
mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa
alikuwa amevalia sketi fupi sana.
Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho
wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya
kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa
mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo
ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo
zake na wanaume katika kituo cha magari ya
abiria kati kati mwa Nairobi.
Maandamano hayo yamefanyika chini ya kauli
mbiu 'My dress my choice'
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii,
wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo
hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke
yanamhusu nini mwanamume ambaye sio
mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha
kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo
alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua
nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi
yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume
wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe
nguzo zao.
LIKE page yetu MJUMBE BLOG au Tutembelee Mtandaoni andika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo upate Picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa Muhimu kila mara.
©Mjumbe Blog Volunteers
Post a Comment