FILIKUNJOMBE AUSAMBARATISHA UKAWA LUDEWA WASHINDWA KUHITIMISHA KAMPENI!
Mbunge wa Ludewa mjini Mhe.Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Ludewa Mjini wakati wa Kufunga kampeni
Wananchi wa Mjini Ludewa waki mshangilia mgombea aliye kuwa akijinadi ndugu John Omary Kiowi
Na Mzee wa matukio daima
FILIKUNJOMBE AUSAMBARATISHA UKAWA LUDEWA WASHINDWA KUHITIMISHA KAMPENI , CCM YAPITA BILA KUPINGWA VITONGOJI 200 KATI YA 352 ,..........
Imewekwa na mzee wa matukiodaima habari bila uoga
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ludewa mjini leo wakati wa kufunga kampeni za CCM
Wananchi wa kijiji cha Ludewa mjini wakimshangilia mbombea wao wa nafasi ya kiti Bw John Omary Kiowi hayupo pichani wakati akiweaomba kura
katibu wa CCM ludewa Eliud Shemauye akimsikiliza mgombea wa kiti ludewa mjini
Wananchi wakimshangilia mgombea wa kiti Ludewa mjini
Mlezi wa UWT mkoa wa Njombe Dr Suzana Kolimba akiwahutubia wananchi wa Ludewa mjini leo wakati wa kufunga mkutano wa kampeni za CCM.
....................................................
WAKATI kesho watanzania kote nchini wanashiriki katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa kuwachagua wenyeviti wa vijiji,mitaa ,vitongoji na wajumbe wake ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewapongeza wananchi wa Ludewa kwa kuwapitisha bila kupingwa wagombea wote wa vitongoji 200 kati ya 352 na vijiji 30 kati ya 77 wagombea wake kupita bila kupingwa .
Huku mbunge Filikunjombe wa kufunga kampeni za CCM kijiji cha Ludewa mjini ukisambaratisha mkutano wa umoja wa vyama vya UKAWA katika kijiji hicho baada ya kuamua kufunga kampeni kimya kimya bila ya kuitisha mkutano kama walivyopanga kuhitimisha mkutano wao eneo la stendi kuu ya Ludewa takribani mita 200 na eneo la Sokoni ambalo mkutano wa CCM ulihitimishwa
Pamoja na ushindi huo wa ngazi za vitongoji na vijiji ambao chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa imeupata kabla ya uchaguzi bado mbunge Filikunjombe amewataka wananchi wa Ludewa kumchagulia wagombea wa CCM ili kufanikisha kuungana nao katika kuleta maendeleo zaidi ya jimbo la Ludewa.
Mbunge Filikunjombe katika mkutano huo wa ufungaji wa kampeni za CCM aliambatana na viongozi mbali mbali wa wilaya na mkoa akiwemo mlezi wa UWT mkoa wa Njombe Dr Suzana Kolimba , katibu mwenezi wa mkoa wa Njombe Honaratus Mgaya pamoja na viongozi wa CCM wilaya hiyo ,Filikunjombe alisema kuwa faraja yake kuona wananchi wa Ludewa wanaendelea kuunga mkono jitihada za CCM pamoja na kazi mbali mbali za kimaendeleo ambazo amekuwa akiwafanyia katika jimbo hilo.
"Ndugu zangu wana Ludewa kwanza niwapongeze kwa kukiwezesha chama cha mapinduzi kuibuka kidedea katika vitongoji 200 kati ya 352 na vijiji zaidi ya 30 kati ya 77 .....kweli mmeonyesha kuniheshimu sana kwa kutambua mchango wangu kwenu nasema ahsanteni kwa kutoniwekea upinzani "
Filikunjombe alisema kuwa ameendelea kuwa na imani kubwa na wananchi wa Ludewa na kuwa lengo lake kuona maendeleo ya jimbo la Ludewa yanaendelea kusonga mbele na ili kufanikisha hayo ni lazima kumchagulia viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji na vijiji kutoka CCM na mwakani katika uchaguzi mkuu basi kumchagulia madiwani wa CCM.
Alisema kuwa ameendelea kuhakikisha ahadi zote alizopata kuzitoa zinatekelezwa ili kuwafanya wananchi wa Ludewa kuzidi kuwa na imani na serikali yao ya CCM chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete .
Hata hivyo alisema kuwa wapo baadhi ya wapinzani katika wilaya hiyo ambao wamekuwa wakijinadi kupitia jina lake kwa madai kuwa wao wapo pamoja na mbunge kwa kuwa mbunge ni mpinzani sio CCM jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwa yeye ni mbunge wa CCM na anayafanya yote kwa nguvu ya CCM na sio upinzani hivyo wananchi wanapaswa kuwapuuza wapinzani kwa kuchagua viongozi wa CCM.
Awali katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eliud Shemauye aliwaeleza wananchi hao kuwa CCM imeanza kusherekea ushindi wa uchaguzi huo hata kabla ya matokeo kutokana na imani kubwa iliyoonyeshwa kwa vitongoji 200 kati ya 352 kwa kuwaacha wagombea wa CCM kupita bila kupingwa pia katika vijiji zaidi ya 30 kati ya 77 ambazo pia CCM imeshinda .
Katibu huyo alisema hadi sasa CCM imemkataa msimamizi msaidizi wa uchaguzi tawi la Milo kijiji cha Milo Bw Endrew Haule baada ya kuungana na wafuasi wa chadema tawi hilo kufunga ofisi ya CCM kwa madai kwa kuzuia shughuli za CCM kufanyika juzi kabla ya msimamizi mkuu wa uchaguzi kuagiza kufunguliwa .
******************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Na Fransis Godwin


.jpg)
Post a Comment