
Habari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga
zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio
Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo .
Habari hizi zinakuja dakika chache baada ya
Millardayo.com kuripoti tetesi zinazohusu8
mustakabali wa kocha huyo Mbrazil.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi
wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja
mkataba wake baada ya kushindwa
kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu
hiyo kwenye masuala ya ufundi .
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri
mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa
kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo
ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
Nafasi ya Maximo sas aitachukuliwa na
Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye
aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu
baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie
Ernst Brandts .
Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga
kufukuza makocha baada ya kufungwa na
Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe
baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts
msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele
ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko
logarusic.
©Mjumbe Blog Volunteers
posted from Bloggeroid
Post a Comment