Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka..
Kituo cha habari cha CBN kimetaarifu kuwa huenda ndege hio imedondokea baharini
Kituo cha habari cha CBN kimetaarifu kuwa huenda ndege hio imedondokea baharini