Unknown Unknown Author
Title: JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA WANAO FANYA FUJO KATIKA ZOEZI LA UAPISHAJI WA VIONGOZI SERIKARI ZA MITAA!!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakifanya fujo katika zoezi la uapishwaji viongozi wa Serikali...

Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakifanya fujo katika zoezi la uapishwaji viongozi wa Serikali za mitaa kwa madai kuwa hawakushinda kihalali katika uchaguzi huo jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi. Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la polisi SSP-Advera Bulimba ambapo amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu ama kikundi chochote kitakachofanya vurugu ama fujo kwa kisingizio cha ushabiki wa siasa na badala yake atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Amesema Tabia hiyo imekuwa ikipelekea kutokea kwa matukio ya watu kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kufanya fujo na vitendo vya vurugu ikiwemo kuwapiga baadhi ya watendaji wanaosimamia zoezi la kuapisha na kuwapiga viongozi wateule waliochaguliwa kihalali na wananchi na badala yake kama mtu hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo,afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake kwenye ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria. Aidha ameongeza kwa kuwataka Wakurugenzi na Maafisa watendaji wenye dhamana ya kusimamia mchakato wa kuwaapisha wenyeviti waliochaguliwa,kufuatilia kwa karibu migogoro inayojitokeza na kuitatua migogoro hiyo mapema ili kuepusha migongano inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top