Unknown Unknown Author
Title: TAFAKARI YA "MIMI MWANAKIJIJI":NA KUWEZA KUMTOA MTU PORINI,NA UKASHINDWA KULITOA PORI LILILO NDANI YAKE!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mimi Mwanakijiji · Neno la tafakari: Hakuna kutawaliwa kubaya kama kutawaliwa kifikra. Ukisoma historia ya ukoloni na utumwa utaona...

Mimi Mwanakijiji · Neno la tafakari: Hakuna kutawaliwa kubaya kama kutawaliwa kifikra. Ukisoma historia ya ukoloni na utumwa utaona kuwa msingi wake mkubwa ni kutawaliwa kifikra; na watawala walitumia muda na nguvu kubwa sana kuhakikisha kuwa watawaliwa waliamini wanastahili kutawaliwa hivyo. Wanapotokea watu katika historia kama Martin Luther King Jr, Mohtma Gandhi, Nelson Mandela, Julius Nyerere, Steve Biko, Patrice Lumumba n.k wanatokea wakija na mawazo ambayo yanagongana kabisa na mawazo ya watu wengi. Iliwachukua muda kuwaaminisha ndugu zao kuwa fikra zinazowatawala zimefika kikomo. Mtu anapotawaliwa kifikra anaweza kabisa kujikuta anaamini watawala wake wanapomtendea vibaya, kumuumiza, kumfanya awe duni bado wanafanya hivyo kwa sabbau wanamtakia mambo mazuri na akisubiri sana siku moja atayapata! Ni vigumu sana kumfungua mtu kifikra; ni rahisi zaidi kufungua minyororo ya mtumwa toka mikono na miguu yake kuliko minyororo ya utumwa katika fikra zake! Unaweza kumtoa mtumwa utumwani lakini usiweze kuutoa utumwa ndani ya mtumwa! *********************************************************************************************************************************************************** Naam;Na Ndipo wazungu walipo sema You Can Remove a person out of the Bush... But you can not Remove a bush within Him!!! ___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________ Maelezo yote Na Mimi Mwanakijiji,Picha Na Maktaba ya MJUMBE BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top