Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo akiwaomba Wananchi wasogee eneo la Mkutano ili kukamilisha zoezi la kuwa apisha wajumbe na wenyeviti walio wa serikari za mitaa waliochaguliwa Mwaka jana.
Kauli ya moja ya viongozi waandamizi wa Serikari walio andamana na Hakimu wa Wilaya ya Momba na Mbozi ili zua Taharuki na kuchafua hali ya hewa na kusababisha Mvutano mkali.
Viongozi waandamizi wa Serikari wakishirikishana jambo baada ya sinto fahamu hiyo ya wana nchi wa kijiji cha Mlowo kutokubali wajumbe na wenye viti wao kuapishwa kwa kile walicho dai ni upotoshwaji wa taarifa iliyo tolewa na moja ya viongozi hao,Aliye sema kuwa "....leo tuta waapisha wajumbe na wenyeviti wa mitaa tu,suala la mwenyekiti lilisha malizika kwasababu alipita bila kupingwa..." tungo iliyo zua Tafaruki kubwa.
Wananchi wa kijiji cha Mlowo wakiwa katika Mvutano mkali na badhi ya viongozi hao na kusisitiza kuwa wafute kauli ili zoezi la kuwa apisha wajumbe na wenye viti hao liendelee,Vinginevyo hawatakubali wajumbe na wenyeviti wao waapishwe mbele yao kwani itakuwa ni kama kushiriki kubariki maovu.
Viongozi waandamizi na baadhi ya wananchi wakibadilishana mawazo ili kunusuru hali ya hewa iliyo kuwa imesha chafuka eneo hilo
Moja ya wajumbe ambao walipaswa waapishwe leo akiwaomba wananhi wawe wasikivu,Hapa alitoa tamko la mkurugenzi wa wilaya ya Mbozi,ambaye alitoa maagizo kuwa zoezi la kuwa apisha wajumbe na wenye viti hao liendelee na kusema kuwa Suala la Mwenyekiti wa kijiji cha Mlowo lipo Mahakamani hivyo hapo sio mahala pake kulizungumzia
Pichani ni Zoezi la Uapishwaji likiendelea baada ya hali ya kuelewana baina ya viongozi hao waandamizi wa kiserikari na wananchi wa kijiji cha Mlowo,Pichani ni jinsi zoezi hilo lilivyo endeshwa na Picha ya Mwishi kabisa chini ni Hakimu wa Wilaya Ndg Kennedy Mloso,Akitoa baadhi ya Maelekezo kwa Wajumbe hao na Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo ambayo itatakiwa ayafute na Mtendaji Kata ili kukamilisha zoezi zima.
Viongozi wandamizi wa Kiserikari wakipongezana baada ya kukamilisha zoezi la kwa apisha viongozi hao kwa amani kijijini hapo
_________________________________________________________________________________________________________________________________
Picha zote na Maelezo na Mdau wa MJUMBE BLOG aliye kuwepo eneo la Tukio
Post a Comment