WALIOTEMBEA KUTOKA GEITA HADI DAR WAZUIWA KUMWONA RAIS
Vijana watatu wa CHADEMA waliotembea kwa miguu kutoka Geita hadi Dar es Salaam kumwona Rais wamewasili jijini Dar es Salaam leo.
Vijana hao walitaka kumwona Rais ili kuwasilisha ujumbe wao ikiwemo kutoridhishwa na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi.
Hata hivyo vijana hao wamezuiwa kumwona Rais kutokana na kutokufuata taratibu za kumwona Rais ikiwa ni pamoja na kutokuomba vibali husika.
Akieleza maamuzi hayo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema "Kuna utaratibu wa kumwona Rais uliotakiwa kufuatwa. Pia kama wametembea kutoka Geita bila vibali husika basi wamefanya kosa la kisheria."
Vijana hao wakiwa wame shikamana mikono
vijana hao wanachama wa chadema wameshaingia jiji la dar es salam wakiwa wamevalia nguo za magunia kuashilia majonzi kwa taifa.vijana hawa wamebeba ujumbe wa
1.ufisadi unavyoligharimu taifa
2.ukiukaji wa haki za binadamu
3.matumizi mabaya ya madaraka kwenye ofisi za umma
police wametanda sehem mbalimbali za ikulu na barabara zote zinazoingia ikulu,
_________________________________________________________________________________________________________________________________
SOMA ZAIDI...
Vijana watatu kutoka nzega wametembea kwa miguu kwa siku 37 hadi jijini dar es saalam kwa lengo la kutaka kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malamiko yao ikiwenmo kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubadilifu wa rasilimali za umma lakini safari ya vijana hao ikaishia mikononi mwa polisi baada ya kukadi agizo halali la mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Jordan Rugimbana la kuwataka wafuate taratibu za kumuona kiongozi huyo wa nchi.
Vijana hao ambao walivamia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za taifa zisivyowanufaisha wazawa.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia matembezi hayo wamewataja vijana hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha kijasiri kama hicho.
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo naye ambapo mkuu huyo aliwtaka wafuate taratibu za kumuona rais na kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo hilo na kusema wao bado ni yao ya kwenda ikulu Ipo pale pale na ndipo walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kablya ya kukamtwa na kupelekwa kituo cha polisi magomeni.
Post a Comment