Pichani ni Mheshimiwa JOSEPH MBILINYI,Alimaarufu SUGU Mara baada ya kunusurika ajalini kwenye mlima kitonga
Picha nyingine,
***********************************************************************************************************************************************************
Kwamjibu wa chanzo chetu,Ajali hiyo imetokea eneo la Kitonga leo mara baada ya gari aliyo kuwa akitumia SUGU Kufeli breki na dereva ndipo alipo amua kuligongesha gari hilo kwenye Ukuta wa mlima/mteremko kitonga badala ya kuligaragazia korongoni ambako ilikuwa ni hatari zaidi.
Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake Kwame Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
“Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu tumepona.
MBUNGE SUGU APATA AJALI KITONGA IRINGA
Mbunge wa mbeya mjini mr sugu akiwa na rafiki yake kando ya gari lao baada ya kupinduka katika mteremko wa kitonga leo.
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph mbilinyi a.k.a Mr Sugu kupitia chama ca demokrasia na Maendeleo[CHADEMA]amenusurika kifo baada ya gari lake kupinduka katika mlima kitonga wilaya ya kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa -Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea mchana wa leo wakati gari hilo likiwa na watu wanne likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es salaam,na hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan\ Mungi amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo japo amesema taarifa kamili itatolewa na askari polisi waliokwenda katika tukio hilo la ajali.
Post a Comment