Unknown Unknown Author
Title: UDASA NA ITV KUANDAA MIDAHALO YA WAGONBEA URAIS 2015!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
1. Katika nchi za kidemokrasia, midahalo ya wagombea imekuwa ni sehemu muhimu katika kufanikisha uchaguzi ulio huru, haki, wazi na amani...

1. Katika nchi za kidemokrasia, midahalo
ya wagombea imekuwa ni sehemu
muhimu katika kufanikisha uchaguzi ulio
huru, haki, wazi na amani. Midahalo hutoa
fursa muhimu kwa wagombea kueleza
falsafa, sera na mikakati yao ya kutatua
matatizo mbalimbali yanayowakabili
wananchi na nchi zao.
Aidha, midahalo huwapa fursa ya kipekee
wapiga kura na wananchi kwa ujumla
katika kuwajua na kupima umahiri na
weledi wagombea na vyama vyao. Kwa
sababu hii, midahalo imekuwa ni sehemu
muhimu ya uchaguzi katika nchi
zinazoamini na kuzingatia misingi ya
demokrasia.
Tafiti zinaonyesha kuwa midahalo ya
wagombea urais ina nafasi ya kipekee
katika kuwawezesha wapiga kura kuamua
mgombea gani wamchague na kwamba
midahalo imekuwa ni chombo muhimu
katika kuhamasisha wananchi kujitokeza
kupiga kura kwa wingi.
2. Kwa kuzingatia msingi ulioelezwa hapo
juu, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) na ITV/
Radio One wamekubaliana kuandaa
midahalo ya wagombea urais kuelekea
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Tunaamini kwamba kwa kuandaa
midahalo hii taasisi zetu hizi mbili
zitakuwa zimetoa mchango muhimu wa
kijamii katika kufanikisha uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top