Unknown Unknown Author
Title: NAIBU SPIKA ANUSURIKA KICHAPO....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BREAKING NEWS, NAIBU SPIKA JOB NDUGAI ANUSURIKA KIPIGO, KISA HIKI HAPA Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya...

BREAKING NEWS, NAIBU SPIKA JOB
NDUGAI ANUSURIKA KIPIGO, KISA HIKI
HAPA
Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia
kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia
Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph
Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano
wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM
Hayo yametokea jana mnamo saa saa 10
jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini
Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera
na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea
nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo
la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa
Bunge La Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa
alipiga kwa gongo ambalo amekuwa
akitembea nalo huku wasimamizi wa
uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha
mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye
kampeni.

Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu
tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea
mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye
ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na
kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo
halijafaidika na chochote kutoka kwa
wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai
alimtishia kuwa anyamaze la sivyo
angemuonesha kazi kwa kile anachodai
kuwa ni kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea
kujibizana suala hilo ndipo ghafla
mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa
wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani
ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa
akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia.

"Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi
sana, unanirekodi na makamera yako na leo
utanitambua mimi ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga
Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata
baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata
na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na
hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka
kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na
ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na
kukimbi Eneo la Tukio.

Inasadikiwa yule
mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr.
Pale chini, jambo ambalo baadhi ya
wananchi walilichukulia ni kama kutaka
kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa
kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi
watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio
hilo ovu mkutano ulivurugika.
Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana
na watu walimbeba akiwa amezimia na
kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3
toka polisi.

Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr
alikuwa bado hajazinduka na madaktari
walikuwa wanaendelea na harakati za
kuokoa maisha ya mgombea huyo.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa
tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi
huo utatumika katika kumuengua Ndugai
katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge
kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia
wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini
bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia
macho.

Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa
kama haki itatendeka Ndugai atakuwa
amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia
KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA
JIMBO LA KONGWA..

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top