Mtu ndani ya sanduku
Maafisa wa polisi nchini Uhispania wamemkamata raia mmoja wa Morroco baada ya nduguye ambaye alikuwa anasafrishwa hadi nchini Uhispania ndani ya sanduku kukosa hewa na nusra afariki.
Watu hao walikuwa wakiabiri feri kutoka eneo la Uhispania la Melilla kaskazini mwa Afrika hadi katika mji wa Bandari wa Almeria kusini mwa Uhispania wakati mzee huyo alipogundua kwamba nduguye hapumui na kuwashauri wafanyikazi wa feri hiyo.
Licha ya kujaribu kumfufua mtu huyo alifariki.
Maafisa wa polisi wamemshtaki nduguye ambaye alikuwa akisafiri kwa kutumia pasipopti ya Ufaransa kwa mauaji ya kutokusudia.
Chanzo:bbc
Post a Comment