Mdau wetu na mtembeleaji wa MJUMBE BLOG tuendelee kuongezana maarifa kwa njia ya mtandao;kupitia hapa kwenye ukuta wetu pendwa.
Leo tena kuna kitu kipya tume kuwekea hapa;
Zifahamu kazi kuu za RITA:
1. Kusimamia Mirathi.
2. Kusajili Vizazi na Vifo na kutoa Vyeti vya Vizazi
na Vifo
3. Kutayarisha takwimu za Vizazi na Vifo.
4. Kutoa Leseni za kufungisha ndoa kwa viongozi
wa dini ( mapadre, Wachungaji, Masheikhs n.k.)
5. Kutoa vibali maalum vya kufunga ndoa bila
kutangaza siku 21
6. Kutoa vibali kuruhusu ndoa kufungwa mahali
maalum ( e.g. hotelini, hospitali n.k )
7. Kusajili ndoa na kutoa nakala za Shahada za
ndoa
8. Kutoa Shahada ya kutokuwepo pingamizi la
ndoa
kwa raia wa Tanzania (mkazi wa Tanzania Bara)
anayetaka kufunga ndoa nje ya nchi
9. Kusajili na kutoa Hati ya Muunganisho kwa
wadhamini wa Vyama vya Siasa, Vikundi,
makanisa, Miskiti na Mali
10.Kusajili watoto wa kuasili na kutoa Hati za
kuasili.
11.Kusimamia mali isiyokuwa na mwenyewe au
ya
watu walio chini ya umri wa utu uzima.
12.Kufanya shughuli za ufilisi na upokezi rasmi
Kusajili makubaliano (Deeds of Arrangements).
Credit:Rita Tanzania.
Share na LIKE ukurasa wetu wa MJUMBE BLOG facebook ili kupanua wigo wa wa familia yetu zaidi.
Post a Comment