Pichani ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi
Saed Kubenea akiyatambulisha
matoleo ya Magazeti mwanahalisi yaliyosababisha Gazeti kufungiwa
picha na Maktaba
Saed Kubenea akiyatambulisha
matoleo ya Magazeti mwanahalisi yaliyosababisha Gazeti kufungiwa
picha na Maktaba
MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara
hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI
Julai 30 miaka mitatu iliyopita. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).
Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.
Katika
uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa,
Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.
Jaji huyo
amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao yote
iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa Waziri –
prerogative orders.
Miongoni
mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia
kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa
kifungoni.(P.T)
Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.
Habari
hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili,
ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi
karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania
(TMA), Dk. Steven Ulimboka.
Dk.
Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo la
Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa
na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa
na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo
siku yatukio.
Daktari
huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la
Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya
tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI,
Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.
Kufuatia
habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema
amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha
kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria
ilizoahidi kuzilinda.
“NImefurahi
sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti.
Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa
kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri
nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.
“Lakini
pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi
kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria
zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni
sheria kandamizi,” alisema.
Mhariri
amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni
ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka
iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku
ya Jumatano.
Kwa muda
wote ambao gazeti hilo linatumikia kifungo, viongozi waandamizi
serikalini, akiwemo rais Jakaya Kikwete, wamekuwa wakitamba kuwa
hawatavumilia gazeti linalochapisha habari za uchochezi.
SOMA ZAIDI:
HATIMAYE
Mahakama kuu imelifungua rasmi Gazeti la Mwanahalisi ambalo lilifungiwa
na serikali kwa mda usiojulikana .Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Akizungumza na Fullhabari.blogs, Mhariri wa Gazeti la Mwanahalisi
,Jabir Idrisa amethitisha kuwa Jaji wa mahakama kuu Salvatory
Bongole,amelifungulia Gazeti hilo na kulitaka liendelee na kazi yake ya
kuhabarisha umma baada kubainika katika kulifungia kwake kanuni
zilikiukwa.
Amesema hukumu hiyo imetokana na kesi namba 27 ya mwaka 2013 ambapo
Kampuni ya Hali halisi limited ambao ni wachapishaji wa Gazeti la
Mwanahalisi walikuwa wakitaka patio la hatua ya waziri wa Habari Fenera
Mukangala juu ya kulifungia Gazeti hilo, Katika kesi ambayo
iliwakilisha kwa Upande wa Serikali na ofisi ya Mwanahseria mkuu wa
Serikali
Jabir
amesema Mahakama imebaini waziri wa Habari hakufuata sheria katika
kulifungia gazeti hilo,licha ya kuwa na mamlaka ya kutokana na sheria ya
Kandamizi ya Magazeti ya mwaka 1976 inampa uwezo wa kulifungia
gazeti,
Amesema Sheria iyo inamtaka waziri husika kufuata hatua kabla ya
kulifungia Gazeti ambapo hatua hiyo ni kuwafuata wale anawaowatuhumu ili
wapate utetezi na kuchukua hatua lakini waziri huyo alipolifungia
Gazeti hilo hakufuata hatua hizo.
HATUA GANI INAFUATA BAADA YA HUKUMU HIYO.
Mwandishi
huyo mwandamizi amesema kwa sasa kinachofuata ni kutaka fidia toka
serikalini juu ya hasara iliyopatika wakati Gazeti hilo lilipokuwa
limefungiwa huku akisema mahakama imeamulu wafanye hivyo.
Amesema Chengine kinachofuata ni mwenyewe Mmiliki wa Gazeti hilo
akiamua kuchapisha Gazeti hilo anachapisha au aache kutokana na
mahakama hiyo kumruhusu.
Kufunguliwa
huko kwa Gazeti la kiuchunguzi la Mwanahalisi kunakuwa ni kama ushindi
kwa Mkurugenzi wa Gazeti Saed Kubenea Mara kwa mara amekuwa ikidai
serikali kulifungulia Gazeti hilo kimakosa……………………………
Post a Comment